Baraza
la Wafamasia Nchini kwa kushirikiana na wafamasia wa Mkoa wa katavi
wamelifungia Duka la dawa muhimu la Semiwe Phamarcy ltd lililoko mjini
Mpanda kwa muda usiojulikana kutokana na Phamarcy kukiuka Sheria
kanuni na taratibu za uendeshaji wa Phamarcy nchini.
Akizungumzia
sababu zilizosababisha kufungiwa kwa Phamarcy hiyo Mfamasia kutoka
Baraza la Famasi Taifa Idara ya Afya Bi Suma David Jailo amesema kuwa
ni kutokana na Mmiliki wa Phamarcy hiyo kufanya biashara bila kuwa na
kibali cha baraza la Famasi ambapo kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Sababu
nyingine aliitaja kuwa Famasi hiyo ilikuwa haina Mfamasia ambaye ni
mtaalam anahusika kusimamamia Famasi kulingana na Sheria za Baraza la
Famasi,ambapo mtu anayefungua Famasi kama hiyo inatakiwa ifunguliwe na
ipate kibali kutoka Baraza la Famasia lakini yeye hakufanya hivyo
wakati akijua taratibu.
Jailo
ameleza kuwa kwa sababu hiyo amefanya makosa kwa kwa kukiuka taratibu
hvyo kwa makosa hayo yote yaliyokutwa kwenye Famasi hiyo imebidi hatua
za awali kuchukuliwa za kuifungia wakati taratibu nyingine za kumfikisha
kwenye mamlaka za kisheria zikiendelea.
Akifafanua
zaidi Mfamasia huyo kutoka Baraza la Famasi Jailo alieleza kuwa Kwa
kuwa sheria wameivunja dawa zote zinakusanywa na kupelekwa kituo cha
Mkoa kwa Mkurugenzi ili taratibu za kisheria zifuatwe.
“Duka
limekutwa na dawa nyingi ambapo kisheria haziruhusiwi kuwepo katika
eneo hili “alisema akaongeza kuwa kwa hili tunatoa ushauri kwa maduka
mengine yeyote yahakikishe kuwa yanakuwa na vibali na yafuate sheria
zilizowekwa na siyo kufanya kama dukua hili ambalo limekutwa na dawa
nyingi amabazo haziruhisiwi kuwepo eneo hili”alisema Suma Jailo.
Akizungumzia
Jamii ya wanakatavi waliokuwa wakihudumiwa na Duka hili na wale
waliokuwa wakifanya kazi hapo na kupata ujira na hasa watumiaji wad aw
alieleza kuwa watu wa maeneo haya watakuwa wameathirika kwa kuwa
walikuwa wakitegemea dawa hizo kuwahudumia hata hivyo kwa upande
mwingine akaeleza kuwa hatua iliyochukuliwa ni saahihi kwa sababuwatu
walikuwa wanapata dawa ambazo siyo sahihi kwa magonjwa waliyokuwa nayo.
Akaongeza
kuwa kwa hivyo kwa njia moja au nyingine wameepusha madhara makubwa
ambayo yangeweza kuwapata watuamiaji ingewezekana mtu akapata dawa
amabayo siyo sahahihi kwa magonjwa aliyo nayo.
Kuhusu
wafanyakazi waliokuwa wakifanya kazi katika Famasi hiyo alisema watoa
huduma wote waliokuwa ni wahudumu na manesi watupu wauzaji ambao hawana
utalaam hakukuwa na Mtaalaam wa kuweza kulingana na ukubwa wa Famasi
hiyo anatakiwa awepo mfamasi mwenye sifa sitahiki.
Alisikitishwa
kuona kuwa Mmiliki wa Famasi hiyokuwani mfamasia na shreia zote za
kuanzisha Famasi anazifahamu na ameishaelezwa na kwa kuwa kilakitu
alichofanya ni kosa kulingana na sheria za Baraza la Famasi atapelekwa
kwenye Priminari Commity ambapo atachukuliwa hatua za kisheria kulingana
na sheria zao.
Kwa
upande wake Kaimu Mfamasia wa Mkoa Katavi kutoka ofisi ya Katibu Tawala
Mkoa wa Katavi Gabriel Changula ameleza kuwa zoezi hilo litakuwa
endelevu na wao wapo kwa ajili ya kusimamia sheria zilizopo na
kuwaondolea wasiwasi wananchi kuwa wasiwe na hofu kutokana na dawa
walizotumia serikali ipo kwa ajili nya kuweza kusimamia sheria na kutoa
maelekezo kwa wananchi wake.
Naye
Mfanyakazi katika Duka hilo aliyejitambulisha kwa jina la MWITA Mitiro
alioneshwa kushangazwa na maamuzi yaliyochukuliwa kwa kuwa haamini nkama
kweli mmiliki wa Duka hilo anaweza kufungua duka bila kuufuata sheria
wakati yeye ni Mfamasi na anaelewa taratibu zote za kufuata.
Akaongeza
kuwa kufungwa kwa duka hilo kwa njia moja au nyingine kumewathiri watu
wengi wanaotegemea huduma ya dawa katika duka hilo kwa kuwa lilikuwa
likisaidia watu wengi tena kwa gharama nafuu na pia kwa upande wa watu
waliokuwa wanafanya kazi hapo familia zao zitateteleka kwa kuwa kibarua
sasa kimeingia mchanga hawana kazi tena kwa muda ambaop watakuwa
wamelifunga duka hilo la dawa ni vyema busara ingetumika kuangali apande
zote mbili bila kathiri upande mmoja au mwingine na akashauri kama
wangeweza kumwita mmliki na kumpatia maelekezo aweze kurekebisha pale
palipo na makosa kuliko hatua zilizochukuliwa.
Na Kibada Kibada – Mpanda Katavi
Chanzo;Full shangwe blog
No comments:
Post a Comment