Wachimbaji wa madini wa mkoa wa katavi wakiwa kwenye mafunzo ya siku nne yaliyoandaliwa na taasisi ya mizinga ya mkoani morogoro iliyochini ya jeshi la ulinzi la kujenga taifa wakifundishwa namna ya kulipua mashimo ya miamba ya madini kwa kutumia baruti mafunzo haya yanafanyika katika ukumbi wa super city mjini mpanda.
picha na walter mguluchuma
Meneja
wa taasisi ya mizinga yenye makao makuu yake mjini morogoro taasisi
inayosimamiwa na jeshi la ulinzi la kujenga taifa PINGU KAMENYI
akifungua mafunzo ya siku nne ya wachimbaji wa madini wa mkoa wa katavi
mafunzo hayo yenye lengo la kuwafundisha namna ya kulipua mashimo ya
miamba kwa kutumia baruti
picha na walter mguluchuma-Katavi yetu Blog
N a Waltel Mguluchuma
Mpanda Katavi yetu blog
Taasisi
ya Serikali ya Mzinga yenye makao yake Morogoro inayosimamiwa na
Wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga Taifa inaendesha mafunzo kwa
washimbaji wa madini wa Mkoa wa Katavi (KARAMA) huu ya namna ya
kulipua miamba ya madini kwenye mashimo kwa kutumia Baruti
Mafunzo
hayo ya siku nne yalifunguliwa hapo jana kwenye ukumbi wa Super City
uliopo mjini hapa na meneja wa mauzo wa Tasisi ya Mzinga bwana Pingu
Kamenyi
Alisema wachimbaji
wengi wanaochimba madini hapa nchini wamekuwa sio wachimbaji rasmi
wa madini kutokana na kufanya kazi nje ya utarabibu
Hivyo mafunzo
hayo yatawapa uwezo wa kufanya shughuli hizo kwa utaalamu hari itakayo
wafanya waongeze pia kipato chao kwa hari hiyo mafunzo yatawaongezea
uwezo
Aliwataka
wachimbaji kuacha tabia ya kuajiri watu waliochini ya miaka kumi
na nane kwenye migogi yao kwani ni sheria inakaza watu chini ya umri
huo kufanya kazi kwenye maeneo yote yanayojishughulisha na shughuli za
uchimbaji wa madini
Kamenyi
aliwaeleza kuwa taasisi ya Mzinga kwa kutambua umuhimu wa
wachimbaji wa Mkoa wa Katavi imeamua kujenga ofisi zake katika eneo la
Misunkumilo ili kuwapunguzia gharama wachimbaji za ununuaji wa baruti
kwani ofisi hiyo itakapofunguliwa watauziwa kwa bei ya chini kuliko
ilivyo sasa ambapo wanalazimika kwenda kununua nje ya mkoa wa Katavi
Kwa
upande wake mhandisi migodi wa kanda ya magharibi Giruad Luyoka
aliwaeleza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia pia kupunguza vifo
vilivyokuwa vikitokea wakati wa ulipuaji wa miamba kwa kutumia baruti
Alifafanua
kuwa wako baadhi ya wachimbaji wamepoteza maisha kutokana na kutoelewa
wasimame wapi wakati wanalipua mashimo ya miamba hivyo mafunzo
haya yatawawezesha wajue mahari pakusimama kwenye maeneo ya usalama
Nae mmoja wa washimbaji hao
Andrea Ikololo alieleza kuwa wachimbaji wengi walikuwa wakipata madini
kidogo kutokana na kutofahamu utaalamu wa kulipua mashimo ya miamba
kwa kutumia baruti hivyo mafunzo hayo yatawaongezea utaalamu kuliko
walivyokuwa mwanzo
Katibu
wa wachimbaji wa madini wa Mkoa wa Katavi (KATAREMA) Joji
Kasanda alisema wachimbaji wamethamini sana mafunzo hayo na ndio
maana idadi yao imeongezeka kutoka idadi iliyokuwa imepangwa ya
washiriki 30 hadi wamefikia 65
Mafunzo
hayo yamewashirikisha washimbaji mbalimbali wa aina za madini
yanayopatikana katika Mkoa wa Katavi kama Vile dhahabu,shaba ulunga na
mengineyo
No comments:
Post a Comment