Na Walter Mguluchuma
Nkasi
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la watu wanaoishi na virusi vya
ukimwi nchini (NACOPHA) Deo Chrispin Mlori ameelezea jinsi vitendo vya
unyanyapaa wanavyofanyiwa na baadhi ya watu katika jamii vinavyoathiri
ufanisi wao wa utekelezaji wa shughuli za kiuchumi na maendeleo kwa
ujumla
Akifungua mkutano wa uchaguzi wa kuunda Baraza la viongozi wa watu
wanaoishi na virusi vya ukimwi liitwalo KONGA uliofanyika juzi mjini
Namanyere katika halmshauri ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa bwana Mlori
alisema waathirika wa ukimwi nao pia wana haki na fursa
sawa ya kuchangia nguvu zao kwa ajili ya maendeleo ya jamii
Alisema kuanzishwa kwa BARAZA hilo la kitaifa lililoundwa kisheria
kwenye mkutano wa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi nchini uliofanyika
mwishoni mwa mwzi Agost jijini Dae es salaam na baadae kuagizwa kuundwa
kwa mabaraza ya wilaya zote nchini ambayo yataitwa KONGA kuna lengo
la kukabiliana na unyanyapaa na ubaguzi unaotokana na hali ya kuishi na
VVU
Bwana Makori aliwaambia wajumbe hao kuwa KONGA zitakazoundwa katika kila
halamshauri ya wilaya zitashirikiana na viongozi wa halmashauri husika
katika kuweka msukumo katika kuratibu na kusimamia uwezeshaji tiba
mafunzo na misada kwa watu wanaoishi VVU na kupinga dhuluma zinazokiuka
utu wa mtu kwa kuunganisha mitandao mbalimbali inayotekeleza program za
ukimwi
Alifafanua kuwa Baraza la kitaifa limeunda timu maalumu itakayoratibu
uundwaji wa KONGA katika halmashauri zote za mikoa ya Rukwa na Katavi
ambapo tayari halmashauri za Manispaa ya Sumbawanga na Sumbawanga mkoani
Rukwa na sasa Nkasi na zile za Halmashauri ya Mji wa Mpanda na
Halmashauri ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavi zimechagua viongozi wake
na kubaki halmashauri za Kalambo (Rukwa) na Mlele na Nsimbo (Katavi)
Wajumbe wa uchaguzi huo walielezwa na mwenyekiti wa halmashauri ya
wilaya ya Nkasi Peter Mizinga ambaye ndiye aliyekuwa msimamizi mkuu
kuwa halmashauri ya wilaya ina wajibu wa kushirikiana na viongozi wa
KONGA hizi katika kuhakikisha kuwa watu wanaoishi na VVU na wengineo
wasiokuwa na virusi kuzuia kuenea kwa maambukizo mapya
Alisema halamshauri ya wilaya ya Nkasi itaanda utaratibu
utakawashirikisha viongozi wa baraz a la wilaya katika kutoa mafunzo kwa
njia ya mikutano semina na makongamano yatakayokuwa yanaendeshwa katika
maeneo mbalimbali kuanzia ngazi za vijiji kata hadi Tarafa na hata
kwenye vikao vya baraza la madiwani wa halmashauri hiyo
Mratibu wa ukimwi katika halmashauri hiyo Filbert Msapila
aliwahahakikishia wajumbe wa kikao hicho na viongozi wake kuwa
ushirikiano wao na halmashauri utawezesha kujenga uwezo wa Taasisi za
watu wanaoishi na VVU ili waweze kumsaidia mtu mmoja mmoja na au
familia zao kupitia program zao
Bi Edinatha Matandiko aliyechaguliwa kwa kura zote 21 za wajumbe
kuongoza baraza la viongozi 10 wa KONGA ya wilaya ya Nkasi alisisitiza
umuhimu wa mitandao yote inayojihusisha na ukimwi chini ya BARAZA la
kitaifa na KONGA za wilaya kusimamia kulinda na kuteteta haki za watu
wanaoishi na virusi vya ukimwi katika jamii na kuwa na mikakati endelevu
ya kukabiliana na maambukizo mapya
No comments:
Post a Comment