Monday, October 28, 2013

MUHONGO AZIAGIZA HALMASHAURI ZIWE ZINATOA TAARIFA KWA WANANCHI YA FEDHA WANAZOZIPATA KWENYE USHURU WA MADINI

Na Walter Mguluchuma

Mpanda Katavi

Waziri wa Nishati na Madini Profesa  Sospeter  Muhongo  amezitaka Halmashauri zote Nchini ambazo  maeneo yao yana migodi ya madini kuhakikisha kuhakikisha wanatowa taarifa za fedha zinazopatikana kutokana na ushuru wa madini kwa wananchi wao

Waziri Muhongo  alitowa kauli hiyo hapo jana wakati akiwahutubia  viongozi wa Mkoa wa Katavi   na wachimbaji wa madini katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi Wa Idara ya maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda  wakati wa ziara yake yasiku mbili ya kukagua miradi ya maendeleo ya Wizara hiyo

Alieleza kuwa wananchi katika maeneo mbalimbali hapa nchini  wamekuwa wakipotosha kuwa  Halmashauri  zimekuwa hazipati ushuru kwenye maeneo yao unaotokana  na ushuru unaotokana na madini kitu ambacho sio sahihi

Alisema hakikisheni mnawasomea wananchi wenu mapato yote ambayo  Halmashauri zenu  zinapata kutoka kwenye makampuni yanayochimba madini badala ya kuwaficha wananchi  na matokeo yake yamekuwa ni wananchi kujenga chuki kwa makampuni hayo wakijua kuwa Halmashauri zao hazipati chochote kutoka kwa makampuni ya uchimbaji wa madini

Pia alizitaka Halmashauri  kuhakikisha fedha  wanazolipwa kutokana na ushuru  wa madini zinatumika kwa ajiri ya shughuli za maendeleo kwenye maeneo yo

Profesa Muhongo alieleza zipo baadhi ya Halshauri wamekuwa wakitumia pesa hizokwa ajili ya watumishi wao  kwenda  kujifundisha namna ya kuzowa taka kwenyw mikoa mingine hayo siyo matumizi mazuri ya fedha alisema Muhongo

Aidha alieleza kuwa serikali imeshaweka utaratibu ambao  hakuna mgodi  ambao unaanzishwa  hapa Nchini bila kuwa na ubia na Serikali  ndio utaratibu ambao  umeisha wekwa na wizara hiyo kwani kama tulikosea mwanzo hatutakiwi kukosea tena

Pia aliwashauri wachimbaji wadogo wadogo  waanzishe vyama vyao  ili iwe rahisi kwao kukopeshwa mikopo ambayo itawasaidia kununua vifaa vya kisasa

Viongozi wa wachimbaji wawe na utaratibu wa kuwasikiliza kero  za wachimbaji  vijijini kuliko ilivyo sasa ambapo wachimbaji wanapiga simu moja kwa moja kwa waziri

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi DR Rajabu Rutengwe alieleza kuwa mbali ya mkoa kuwa na madini mbalimbali kama vile Dhahabu  Shaba  bado wachimbaji wanakabiliwa na changamoto mbalimbali

Rutengwe alizitaja baadhi ya changamoto hizo kuwani vifaa duni  wanavyotumia kuchimbia  na mitaji midogo kwa wachimbaji

Nae Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo wa Mkoa wa Katavi Willy Mbogo alimweleza waziri Muhogo kuwa jumla ya leseni 1035 zimeisha tolewa kwa wachimbaji wadogo wa Mkoa wa Katavi

No comments:

Post a Comment