Wednesday, February 20, 2013

SERIKALI YA MLELE YAPIGA MARUFUKU UUZAJI WA MAZAO KIHOLELA‏


Na Walter Mguluchuma
Katavi
Serikali Wilayani  Mlele Mkoa wa Katavi  imewaagiza  viongozi  wa vijiji  na kata  kuhakikisha  wananchi hawauzi  chakula  cha msimu  huu  bila kufuata utaratibu  ulio  wekwa  unao  wataka wauze  chakula   cha ziada tuu
Kauli hiyo  imetolewa na  mkuu wa  wilaya ya Mlele  kanali Gemela  Lubinga  wakati akiongea na waandishi wa habari  hapo jana  ofisini  kwake
Agizo  hili  alilitowa  kufuatia  msimu  huu  wanancchi  wa wilaya ya Mlele  na mkoa wa Katavi  kuuza mazao yao kwa wafanya biashara  wa mikoa mbalimbali  bila  kuwa na utaratibu wa kujiwekea  akiba ya chakula  cha katosha
Alieleza  kuwa  kitendo  cha wananchi  kuuza  chakula kwa wafanya biashara  kumesababisha  kupanda  kaw gharama  ya bei ya mazao  ya chakula  kwa msimi  huu katika  Mkoa wa  Katavi  tofauti na msimu wa mwaka jana
Alifafanua kuwa  msimu  wa mwaka  jana mwezi kama huu  debe moja la mahindi  lilikuwa likiuzwa kwa  bei ya shilingi  8000 wakati  mwaka huu  mahindi yanauzwa kwa  bei ya shilingi  17000 kwa debe moja
Kanali  Lubinga alieleza  kuwa  kutokana na wananchi  kuuza mazao yao  kiholela  msimu  huu wa mavuno  watendaji wa  vijiji na  kata  katika Wilaya ya mlele  wamekabidhiwa jukumu  la  kuwasimamia  wananchi kwenye maeneo  yao  kuuza mazao  ambayo  yatakuwa na yaziada  na  sivinginevyo
N aviongozi   ambao watakao waruhusu  watu wao kuuza  mazao yao bila kufuata  utaratibu  watachukuliwa hatua  za kinidhamu  kwa kushindwa kutekeleza majukumu  walio pewa
Alisema yeye  kama mkuu wa Wilaya  atakuwa anafanya  ukaguzi  kwenye   baadhi ya  kaya  kwa vipindi tofauti  ili  kufuatilia kama wananchi  wametekeleza  maagizo hayo  yalio tolewa na serikali  ya wilaya ya Mlele
Aidha alisema kuwa  amewashauri  wakulima  wakulima wa wilaya hiyo  kuachana  na kilimo  walicho kizowea    cha kilimo cha matuta  kwani kinawapotezea  nafasi kubwa ya kupanda mimea  mingi na badala yake  walime kilimo  cha sesa
pia alieza kuwa kutokana  na kupanda kwa bei ya mahindi   mkuu wa Mkoa wa Katavi  ameomba  mkoa upatiwe tani 2000 za mahindi  kutoka  kwenye gara la hifadhi ya   chakula     cha Taifa 
Lengo  la kuomba kibali hicho  serikali  ni  kutaka  mahindi  hayo yaliyo ifadhiwa katika magara ya  Mpanda yaweze  kusangwa unga  na wananchi  waweze kuuziwa unga huo wa  mahindi kwa bei nafuu

No comments:

Post a Comment