Na Walter Mguluchuma-BLOGS ZA MIKOA
Mpanda
Majambazi wameliteka gari la mfanya biashara wa duka la dawa muhimu la binadamu wa Mjini Mpanda Mkoa wa Katavi Michael Mpela na kufanikiwa kupora vitu vyenye thamani ya shilingi 480 000.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Katavi Joseph Myovela alisema tukio hilo la uporaji lilitokeaa februari 8 majira ya saa 2 usiku katika eneo la Kijiji cha Sijonga barabara ya Mpanda kuelekea Karema mwambao wa ziwa Tanganyika .
Katika tukio hili majambazi watatu wakiwa na bunduki moja waliliteka gari namba T 595 AGS aina Escudo mali ya Michael Mpela aliye kuwa na wenzake wawili.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Katavi alisema baada ya kuwateka walifanikiwa kuwapora pesa taslimu jumla ya shilingi 240 000.
pia majambazi hao waliwalazimisha kusalisha simu zao za mikononi na waliweza kupora simu tano za aina mbambali zenye thamani ya shilingi 240 000.
Myovela alisema majambazi hayo mara baada ya kufanya ujambazi huo yalitokomea kichakani na kutokomea kusiko julikana .
Alieleza jeshi la polisi linaendelea na msako wa kuwatafuta mambazi walio husika katika tukio hili kwa kushirikiana na wananchi .
Na jeshi la polisi mkoa wa Katavi limetowa wito kwa kwa wananchi kutowa taarifa mapema waonapo watu ambao ni wageni katika maeneo yao wanapo kuwa na mashaka nao kabla hawaja fanya adhima yao ya uharifu
No comments:
Post a Comment