Na Walter Mguluchuma
Mpanda – Katavi
Jeshi la polisi mkoani Katavi linawashikilia watu watatu baada ya kuwakamata na silaha mbili za kivita aina ya SMG, MAGAZINE na RISASI 77
Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari amewataja waliokamatwa na silaha hizo kuwa ni Gervas Zacharia (35) mkazi wa kata ya mamba wilayani Mlele, Peter Abdallah (Ndombo) (29) mkaziwa kijiji cha Miombo wilayani Nkazi na Sebastiano Maembe (52) mkazi wa kata ya Muze wilayani Sumbawanga.
Watuhumiwa hao walikamatwa mwanzoni mwa wiki hii baada ya kufanyika msako mkazli wa kuwatafuta wao ambao waliteka magari mawili na kupora vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi 5,524,000 katika kijiji cha Milumba wilayani Mlele mkoa wa Katavi
Kidavashari alieleza kuwa katika tukio hilo waliteka gari lenye namba za usajiri T9785 STK LAND CRUISER mali ya TANROAD mkoa wa Katavi iliyokuwa ikiendeshwa na Miraji Haji (46) aliyekuwa na watumishi wenzake watatu na waliporwa simu moja aina ya TECNO, simu mbili aina ya NOKIA na simu aina ya BRACKBRRY na fedha taslimu Tsh. 2,420,000/=
Katika tukio jingine siku hiyohiyo ya januari 15 mwaka huu majira ya saa 9:00 mchana katika eneo hilohilo watuhumiwa hao wakiwa wenzao watatu waliliteka gari aina ya FUSO lenye namba za usajiri T336 CBX lililokuwa likiendeshwa na Simon Simtowe (31).
Kidavashari alieleza watu hao walifanikiwa kupora vitu mbalimbali vyenye thamani ya Tsh. 3, 104,000/= na mara baada ya tukio watuhumiwa walitokomea kusikojulikana.
Jeshi la polisi mkoa wa Katavi na Rukwa kwa kushirikiana na raia wema walianza msako mkali wa kuwasaka watuhumiwa.
Kidavashari alieleza katika msako huo walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wa ujambazi hawa watatu wakiwa na silaha mbili aina ya SMG NO. AFU 2911 na SMG NO. TZO 681, MAGAZINE NNE na RISASI 77 chupa moja ya mafuta ya kusafirishia bunduki.
Pia walikamatwa wakiwa na panga moja, simu moja aina ya NOKIA na Camera moja aina ya SONY ambayo ambayo tayari imeishatambuliwa na mwenye mali hiyo.
Kidavashari ameeleza kuwa watuhumiwa baada ya kuhojiwa na jeshi la polisi wamekiri kuwa wamewahi kujihusisha pia katika matukio mengine mbalimbali yaliyowahi kutokea katika mikoa ya Katavi na Rukwa.
Alisema mtuhumiwa wa ujambazi wa tukio hili Sebastin Maembe ndio pia walikuwa wakimtumia kama mganga wao wa kienyeji kwa kuwasafishia nyota zao ili wanapokuwa kwenye matukio ya ujambazi wasiweze kukamatwa.
Kamanda huyo wa mkoa alisema watuhumiwa wote watatu watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Aidha jeshi la polisi mkoa wa Katavi limetowa wito kwa wahnanchi waendelee na moyo wa kushirikiana na jeshi hilo katika kuwafichua waharifu kabla hawajafanya uharifu.
No comments:
Post a Comment