Home » » WANNE WASHIKILIWA NA POLISI KWA KUFANYA VURUGU MSIKITINI YA KUTWANGANA MAKONDE WAKIGOMBEA KUONGOZA IBADA

WANNE WASHIKILIWA NA POLISI KWA KUFANYA VURUGU MSIKITINI YA KUTWANGANA MAKONDE WAKIGOMBEA KUONGOZA IBADA


Na Walter Mguluchuma
Mpanda.
Watu wanne wanashikiliwa na jeshi la polisi wilayani mpanda mkoani Katavi kwa kufanya vurugu msikitini na kusababisha kuvunjika kwa ibada ya Ijumaa.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashar amewataja watu hao kuwa ni Juma Mazomba (32) Ibrahimu Rashid (42) Mussa Hamis (27)  Husein Omary (32) wote wakazi wa mtaa wa Kawajense.
Alisema watu hao walifanya vurugu hizo hapo juzi majira ya saa 7:15 mchana katika msikitii wa Kawajense Namba mbili.
Katika tukio hilo watu hao kila mmoja alikuwa akidai yeye ndiye mwenye uharali wa kuendesha (kuongoza) ibada ya Ijumaa katika msikiti huo,
Kidavashari alisema mabishano hayo yaliendelea huku waumini wa dhehebu hilo wakiwa wakisubiria kuanza kwa ibada hiyo.
Kamanda Kidavashari alieleza kuwa baada ya kuona ibada imechelewa kuanza na viongozi hao wakiwa wanaendelea na mabishano waumini hao walitaka kujua kile kilichokuwa kikiendelea.
Ndipo ghafla viongozi hao walipoanza kurushana makonde hari ambayo iliwafanya baadhi ya waumini waliokuwa ndani ya msikiti huo wanaoishi jirani kutoka mbio na kwenda kuchukua silaha za jadi na kisha kurudi msikitini hapo.
Hata hivyo polisi walipata taarifa za tukio hilo na waliwasiri muda mfupi na kufanikiwa kutuliza ghassia hizo za pande hizo za viongozi wao wa msikiti.
Alisema kutokana na vurugu hizo zilifanya waumini kutofanya ibada ya Ijumaa katika msikiti huo.
Kidavashari alisema ugomvi huo umesababishwa na watu hao kuwa na uchu wa madaraka kwani kila upande unadai wao ni viongozi harari wa kusalisha katika msikiti huo.
Watu hao wote wanne bado wanaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya kufanya vurugu ndani ya msikiti wakati wa ibada

1 comments:

Mbele said...

Hivi kweli kwa mtindo huu Mungu atasikiliza maombi yetu? Matatizo ya aina hii yamejitokeza pia miongoni mwa wafuasi wa dini zingine. Kazi tunayo.

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa