Na Walter Mguluchuma
Mpanda - Katavi.
WAKAZI wa eneo la Kigamboni lililopo katika kata ya Makanyangio katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali iweze kuwajengea kivuto kutokana na kivuko kilichopo kotohimili mvua za masika zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali hapa nchini na hivyo kuwaweka katika hatari ya kusomwa na maji.
Wakizungumza na Gazeti hili wakazi hao wamesema kuwa kutokuwa na kivuko imara katika eneo hilo la kawajense kumekuwa kukihatarisha maisha yao na maisha ya wagonjwa huku wanafunzi wengi wakishindwa kuhudhuria masomo yao kutokana na kushindwa kuvuka katika eneo hilo lililojengwa daraja la chini na hivyo kuishauri serikali kujenga daraja la juu.
Wakazi hao wamesema kuwa hivi sasa katika kipindi cha mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali hapa nchini kumesababisha daraja hilo kutopitika na hivyo kuwapa wakati mgumu wa kuendesha shughuri zao za kuwaendeshea kipato huku wakiofia pia masiaha yao kutoka na daraja hilo kujaa maji kila wakati.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Makanyagio Bw Iddy Nziguye amesema kuwa mpaka sasa wamekwisha fanya mawasiliano na idara ya ujenzi katika halmashuari ya mji wa mpanda kwa lengo la kunusuru maisha ya wakazi hao ,huku mkurugenzi wa halamshauri hiyo Bw Joseph Mchina akisema kuwa barabara hiyo ipo katika mpango wa ujenzi katika mwaka huu wa fedha,ikiwa ni pamoja na ofisi za wabunge wa jimbo la mpanda mjini.
Bw Mchina amesema kuwa mpaka sasa zabuni ya ujenzi wa barabara hiyo ya kigamboni hadi makanyagio imekwishatangazwa na wakati wowote kaunzia sasa ujenzi wa barabara hiyo pamoja na daraja vitajengwa.
No comments:
Post a Comment