Na Walter Mguluchuma.
Mpanda Katavi.
Makamu Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Taifa Said Arfi ametowa tamko la kuitaka TAKUKURU imchunguze kuhusiana na tuhuma zilizo tolewa dhidi yake kuhusiana na tuhuma za kupokea rushwa kutoka Mizengo Pinda waziri mkuu wa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
tamko hilo alilitowa hapo jana wakati akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara ulio fanyika jana katika mtaa wa mpanda Hotel alikuwa akiwahutubia mamia ya wananchi.
Arfi alitowa kauli hiyo kufuatia tuhuma zilizo tolewa dhidi yake kwenye mkutano wa mashauliano ya mikoa ya Rukwa na Katavi ulio fanyika desemba 16 mwaka huu wilayani Nkasi mkoani Rukwa ambapo alihumiwa waziwazi na mwenyekiti wa BAVICHA wa mikoa hiyo Laulenti wa Mangeshi na kupelekea menyekiti huyo wa BAVICHA kusimamishwa uongozi na mkutano huo
katika mkutano huo wa jana Arfi ambaye ni mbunge wa jimbo la mpanda mjini alisema endepo TAKUKURU itamchunguza na kumuona alihusika na kupokea hongo kutoka kwa Pinda wakati wa uchaguzi mkuu wa 2010 ili kumwezesha Pinda apite bila kupingwa katika jimbo la uchaguzi la Mlele basi akamatwe na afungwe gerezani pia na Pinda akamatwe kwa kumpa rushwa.
alisema kuwa yeye ni mwadilifu na hapendi kuchafuliwa na ndio maana baada ya kushutumiwa kwenye kikao hicho ndiyo siku iliyo fuata ya desemba 17 alikwenda kutowa taarifa zilizo tolewa dhidi yake TAKUKURU ili waweze kuzichunguza kama zina ukweli ndani yake.
alifafanua kuwa taarifa ya uchunguzi huo itakapo kamilika anaiomba Takukuru iweke hadharani na endepo haita thibitika kama hakuhusika hatakuwa na msamaha kwa watu walimtuhumu na yuko tayari kuwalipia ghama ya chakula gerezani pindi watakapo shindwa kumlipa gharama za kumdhalilisha mahamani.
pia alitumia mkutano huo kutowa taarifa ambazo zilikuwa zimeenea na kusambazwa kwenye baadhi ya magazeti kuhusiana na yeye kutupa kadi ya CHADEMA alisema taarifa hizo kuwa sehemu zilikuwa zimeandikwa za ukweli na sehemu hazikuwa na ukweli.
Makamu huyo mwenyekiti wa taaifa alisema yeye bado ni kiongozi wa CHADEMA na kadi yake anayo mwenyewe yenye namba 000063 na ameisha ilipia hadi mwaka 2015 hivyo napenda kuwahakishia wanachi wa mpanda na watanzania kwa ujumla kuwa sija tupa kadi ya chadema.
alisema vijana hata kama wanataka uongozi wafuate tararibu za chama kwani unapo taka uongozi sio lazima umchafue mtu yeye yuko tayari kumpisha kijana yoyote ndani ya chadema ambae ataona ana na kumshinda kwenye kula za maoni.
hivyo aliwaomba vijana vijana watafute mtu mwenye kujieshimu mwenye adabu na mwenye kuheshimu wakubwa a
mkutatano wa mashauliano wa chama hicho ulio fanyika desemba 16 wilayani Nkasi ulileta mgawanyiko ndani ya kikao hicho baada ya kutolewa tuhuma kwa Arfi zilizo anzishwa na mwenyekiti wa BAVICHA zilizo mtuhumu kupokea hongo tukoka kwa pinda aliambayo ilimkasirisha na kutoka ndani ya kikao kile alicho dai awezi kudharishwa na vijana wadogo.
katika mkutano kuu waliamua kumsimamisha wao BAVICHAuongozi baada ya wajumbe kupiga kura za maamuzi ambapo kura 24 zilisema asimamishwe na kura 12 zilipinga
No comments:
Post a Comment