Na Walter Mguluchuma
Mpanda
Mbunge wa jimbo la Mpanda Mjini ambae pia ni makamu mwenyekiti wa taifa waChama cha Chadema amewataka viongozi na wananchi wa mkoa wa katavi waachane na kuendeleza chuki za kisiasa na badala yake wafanye kazi za kuleta maendeleo .
Hayo aliyasema hapo juzi kwente mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye mtaa wa majengo B’ alipokuwa akiwahutubia mamia ya wakazi wa mji wa mpanda.
Alisema wapo viongozi ambao wamekuwa hawatimizi majukumu yao kwa wananchi mkoani Katavi kwa ajiri ya chuku zao za kisiasa.
Alifafanua kuwa hiki kipindi sio cha watu kuendeleza chuki za kisiasa bali ni kipindi cha watu na viongozi kufanya kazi za kuleta maendeleo
Hali ya viongozi kuwa na migogoro na wananchi ya mara kwa mara kama itaendelea hivyo upo uwezekano wa kutokea kwa vurugu kama zile zilizotokea mikoa ya Mwanza na Mbeya
Alisema tabia iliyopo wilayani Mpanda ya migogoro ya mara kwa mara baina ya Halmashauri ya mji huu na wafanya biashara wadogo kama haitapatiwa ufumbuzi upo uwezekano mkubwa wa uvunjwaji wa amnai kutokea.
Alishauri viongozi waache kuchukua baadhi ya maamuzi kwa kutumia mabavu na badala yake wawe na utaratibu wa kusikiliza mawazo ya wananchi.
Mbunge huyo alisema migogoro hiyo ya viongozi na wananchi itakapokuwa inaendelea inawafanya watu waichukie serikali ya chama tawala hari ambayo inazidi kumtengea yeye mazingira mazuri ya kushinda tena kwenye uchaguzi mkuu ujao wa 2015 alisema Arfi.
Pia aliwataka wananchi wa mji wa mpanda waachane na malumbano ya kisiasa kwani muda huo wa kulumbana umeshapita hivyo ni vizuri wakafanya kazi za kuwaletea maendeleo.
Kumekuwa na migogoro ya mara kwa mara baina ya Halmashauri ya mji wa mpanda na wafanyabiashara wadogo wa mji huo toka ulipomalizika uchaguzi mkuu wa 2010.
Migogoro ya Halmashauri ya mji wa mpanda na wafanyabiashara wadogo huenda ukasababisha mahudhurio ya wananchi kwenye sherehe za uzinduzi wa mkoa mpya wa Katavi ukawa na watu wachache.
Sherehe za uzinduzi zimepangwa kufanyika Novemba 25 ambapo mgeni rasmi atakuwa ni Makamu wa Rais wa serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzani Dokta Ghalibu Bilali.
No comments:
Post a Comment