Na Walter Mguluchuma
Mpanda
Watu wawili wamekufa na wengine 16 kujeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka katika kijiji cha Kanoge makazi ya wakimbizi ya katumba wilayni Mlele mkoa wa Katavi
Ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 8:30 mchana katika mlima wa Kanoge na kulihusisha gari Na. TZ78 378 Toyota aina ya Hilux mali ya Mashaka Gewe (Chinga) mkazi wa mtaa wa makanyagio mjini mpanda.
Mganga mkuu wa mkoa wa katavi Dr. Yahaya Hussein aliwataja marehemu waliokufa kuwa ni Hawa Kuyenga (18) mkazi wa kijiji cha Mpanda ndogo na marehemu wa pili bado hajatambuliwa
Dr. Yahaya aliwataja watu 16 walijeruhiwa kuwa ni Sadala Salumu (36), John Joseph (30), Husein Manene (12), Maneno Musa (55) Winifrida Charles (50), wote wakazi wa kijiji cha Ugalla Wilayni Mlele
Wengine wametaja kuwa ni 6,Nyamatondo Kayela (28) Bahati Kalongo (48) Richard Kuyega (39) Zuhura Husein (33) wote wakazi wa kata ya Mpandandogo
Joseph Lupamba (40) mkazi wa mtaa wa kawajense no. II Johari Nassoro (19) mkazi wa kijiji cha Kambuzi,, Stephano Edwrd mkazi wa makazi ya wakimbizi ya katumba na Robart Debo.
Mganga mkuu wa mkoa wa katavi alisema majeruhi hao wote wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Mpanda na kati yao wane hari zao sio nzuri
Miili ya marehemu wote wawili ipo katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya wilaya ya Mpanda ikisubiliwa kuchukuiwa na ndugu zao
Baadhi ya watu walioshuhudia ajali hiyo ya gari ambalo lilikuwa likitokea kata ya ugalla wilaya ya Mlele kuja Mpanda mjini ilitokana na gari hilo kutokuwa na breki na kupelekea kushuka kwa kasi kwenye mtelemko huo mkali wa mlima
Dreva wa gari hilo mara baada ya kutoka ajali hio alitokomea porini na mpaka sasa hivi hajapatikana
Kamanda wa polisi wa mkoa wa katavi Dhahiri Kidavashari amethibitisha kutoke kwa ajali hiyo
No comments:
Post a Comment