Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya akimkabidhi mwenge wa uhuru mkuu wa mkoa wa Katavi, Rajabu Rutengwe makabidhiano ambayo yalifanyika katika eneo la Stalike wilayani Mpanda jana baada ya mwenge huo kumaliza kukimbizwa mkoani Rukwa. Picha na Mussa Mwangoka
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Honest Mwanossa akizungmza na baadhi ya
watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda (hawapo pichani) jana kuhusu
udhaifu wao katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo hali
inayosababisha kujengwa chini ya kiwango pembeni yake ni mkuu wa wilaya hiyo
Paza Mwamlima. Picha na Mussa Mwangoka
Mussa Mwangoka, KataviYetu
UWAJIBIKAJI mdogo na kukithiri kwa rushwa miongoni mwa baadhi ya madiwani na
watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavi ni sababu tosha
inayochangia miradi mingi ya maendeleo kutekelezwa chini ya kiwango.
Kiongozi wambio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu, Honest Mwanossa alisema hayo jana mara baada ya kukagua na kukataa kuipokea baadhi ya miradi ya maendeleo ambayo inapitiwa na mbio za mwenge wa uhuru mkoani humo.
Miradi ambayo aliikataa ni ile ya ujenzi wa ofisi ya Mbunge jimbo la Mpanda vijiji ambayo alidai imejengwa chini ya kiwango ambapo fedha iliyotumika haifanani na thamani ya jengo hilo.

Pia amekosoa ujenzi wa miradi kadhaa na kutaka kasoro
zilizojitokeza ikiwamo kuwa na nyufa zinarekebishwa na wakandarasi
waliotekeleza miradi hiyo haraka iwezekanavyo.
Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge, licha ya kukataa kupokea majemgo hayo pia alimtaka mkurugenzi wa wilaya hiyo kutoa maelez0 ya kina kwanini hali hiyo inajitokeza, huku mhandisi wa wilaya akikacha msafara huo ili kukwepa hoja zilizokuwa zikimkabili kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo.
Alisema kuwa tabia ya baadhi ya watendaji kuchukua asilimia kumi "ten percent" kutoka kwa wakandarasi waliopewa zabuni imekuwa sugu kwa sasa hali ambayo inachangia miradi mingi ya maendeleo kutekelezwa ikiwa chini ya kiwango na kutofanana na fedha halisi inayotajwa kutumika.
Katika hatua nyingine aliwataka madiwani kuacha udhaifu katika kusimamia vizuri rasilimali fedha ndani ya halmashauri zao kwani kutofanya hivyo kunatoa mwanya watendaji wasio waaminifu ambao sasa wamegeuka mchwa na kutafuna rasilimali hizo kwa kutokuwa wazalendo katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mwanossa aliongeza kuwa watendaji wasio waaminifu kamwe hawatafumbiwa macho kwa kuwa ndio wanaoichafua Serikali mbele ya wananchi kwa kutekeleza miradi mibovu, hivyo wanapaswa kubadilika mara moja kabla hatua za kuwashughulikia hazijaanza kuchukuliwa kwani wameanza kufahamika.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa katavi, Dk Rajab Rutengwe, akisoma taarifa ya mkoa baada ya kupokea mwenge kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ,Mhandisi Stella Manyanya katika kijiji cha Sitalike alisema mwenge wa uhuru ukiwa mkoani humo utapitia miradi 34 yenye thamani ya Sh 2,225,855,250- ambayo itakaguliwa kuwekewa mawae ya msingi , kuzinduliwa na kufunguliwa.
Alisema wananchi wamechangia Sh 398,547,241- huku Halmashauri zikiwa zimechangia Sh 1,298,842,859-, wahisani na wadau wengine wa maendeleo Sh 176,265,150- na Serikali Kuu Sh 352,200,000-.
Kwa mujibu wa Dk Rutengwe, baada ya kuhitimisha mbio zake katika mkoa wa Katavi , mwenge utakabidhiwa kwa uongozi wa mkoa wa Tabora Septemba 22, mwaka huu kijijini Ipole katika wilaya ya Sikonge.

Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment