Na Walter Mguluchuma, Mpanda-Katavi yetu
Mwanasheria wa kampuni ya uanasheria ya Marando Mnyele and Advecates yenye makao yake maluum mjini Dar es salaam amechukua fomu ya kugombea ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) katika Mkoa wa katavi.
Mwanasheria huyo Gabriel Mnyele mwenye shahada mbili za sheria alikuwa ni mgombea wa kwanza kuchukua fomu hizo za kugombea nafasi hiyo hapo juzi.
Mnyere ambaye alipata shahada yake ya kwanza mara baada ya kuhitimu katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam hapo mwaka 1992, na shahada yake ya pili alihitimu nchini Uingereza katika Chuo Kikuu cha Warwick na amekuwa wakili wa kujitegemea tangu mwaka 1992.
Mnyere pia ni mwanasheria mkuu wa Chama cha Walimu nchini (CWT).
Mgombea mwingine aliyechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo ni Charles Emmanuel ambaye ni Mwenyekiti wa CCM wa kata ya Makanyagio vilevile ni dreva wa gari la chama hicho Wilaya ya mpanda.
Wakati huohuo mwandishi wa habari ambaye pia ni mwakili wa radio maria mkoa wa Katavi Elias Milwano amechukua fomu za kugombea wa katibu mwenezi wa CCM wa mkoa wa katavi nafasi ambayo inatajiwa pia kugombeawa na katibu mwenezi wa wilaya ya mpanda Joseph Makumbule ambaye toka awali alishatangaza nia hiyo.
Blogzamikoa
No comments:
Post a Comment