Friday, August 24, 2012

ACHOMWA KISU NA KUPORWA PIKIPIKI

Na Walter Mguluchuma, Mpanda-Katavi Yetu
Mwendesha pikipiki (bodaboda) wa mjini mpanda Mkoani Katavi Jastini Farijara ameporwa pikipiki na abiria wake baada ya kuchomwa kisu usoni.
Tukio hili limetokea usiku usiku wa kuamkia jana majira ya saa tatu katika maeneo ya mtaa wa misunkumilo mjini mpanda ambapo abiria huyo alikimbia na pikipiki hiyo kusikojulikana.
Mwendesha pikipiki huyo alikuwa na pikipiki yenye namba za usajili T418 CBO SANLG Mali ya Dezideli Magezi akiwa amepaki pikipikikatika eneo la baa ya Fimbo ya Myonge katika mtaa wa makanyagio akisubiri wateja ndipo alipotekea abiria huyo ambaye hakuwa anamfahamu na kumwomba ampeleke katika eneo la shule ya waschana ya mpanda  iliyoko mtaa wa misunkumilo.
Mwendesha bodaboda Jastini alisema hakuwa na shaka yoyote na mteja wake huyo kwa jinsi alivyo kuwa amevaa nguo za heshima hari ambayo ilimfanya akubaliane kumpeleka kwa gharama ya sh.5000.
Alieleza wakati wakiwa wanaendelea na safari yao kabla hawajafika alikokuwa amemweleza wanako kwenda abiria huyo alimwamuru bodaboda huyo kusimamisha pikipiki na ndipo alipotii agizo hilo kwa lengo la kutaka kusikiliza shida yake.
Hata hivyo baada ya kusimama abiria huyo alichomoa kisu kilichokuwa mfukoni mwake na kuanza kumchoma sehemu za uso huku akimwamuru ashuke kwenye pikipiki.
Alisema ndipo alipokubali kushuka kwenye pikipiki na kisha mtu huyo alichukua pikipiki  hiyo na kutokomea kuiko julikana na huku yeye akiwa amebaki ameduwaa.
Jeshi la polisi wilaya ya mpanda limethibitishwa kupolwa kwa pikipiki hiyo yenye namba  za usajili T418 CBO na mwendesha bodaboda huyo amelazwa katika hospitali ya wilaya yam panda ambapo anapatiwa matibabu
Blogzamikoa

No comments:

Post a Comment