Mwandishi wetu, Katavi Yetu
Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuiwakilisha serikali katika mazishi ya Mhashamu Askofu Pascal Wiilliam Kikoti wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda, aliyefariki dunia juzi kwa shinikizo la damu yatakayofanyika siku ya jumamosi.

Akitangaza ratiba ya mazishi hayo mara baada ya Kikao cha kwanza cha Bodi ya Mfuko wa Barabara ya Mkoa wa Katavi, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dk. Rajab Rutengwe alisema mwili wa marehemu unapokelewa leo kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda na viongozi mbalimbali wa dini na Serikali wa mkoa wakiongozwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Mara baada ya kupokelewa, mwili huo utapelekwa Kanisa la Mt. Maria Imakulata, makao makuu ya Jimbo Katoliki Mpanda kwa taratibu nyingine za kikanisa.
Mhashamu Askofu Pascal William Kikoti alifariki dunia Agosti 28, mwaka huu katika Hospitali ya Bugando, jijini Mwanza na mazishi yake yanatarajiwa kufanyika kesho kutwa (Jumamosi, Septemba mosi, 2012.
Blogzamikoa
No comments:
Post a Comment