Na Walter Mguluchuma, Mpanda-Katavi yetu.
Mwanamke mmoja wa kijiji cha mnyaki Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi ameuwawa kwa kuchomwa na visu porini na kuporwa shilingi milioni 2.5 baada ya kudanganywa na mtu aliyejifanya ni mkulima wa karanga.
Mwanamke huyo ambaye alikuwa mfanya biashara wa zao la karanga ametajwa kuwa ni Consolata Julias (41)
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita majira ya saa 9:30 alasiri katika eneo la kijiji cha Kabatini karibu na mji wa mpanda.
Mume wa marehemu Said Shaban alisema siku ya tukio mkewe alitoka nyumbani kwake majira ya asubuhi kwenda kutafuta karanga za biashara wakati akiwa njia alikutana na mtu mmoja ambaye alimweleza marehemu mkewe kuwa yeye ni mkulima wa karanga na yuko tayari kufanya nae biashara kwa kumuuzia karanga alizohitaji.
Baada ya mazungumzo mtu huyo almtaka marehemu waende eneo la kijiji cha jirani ambako ndiko alidai kuhifadhi karanga hizo na kuondoka na mtu huyo kwa usafiri wa pikipiki wakielekea njia ya mpanda mjini kuelekea Inyonga wilayani mlele
Hata hivyo mtu huyo alipofika katika eneo la kabatini alimwingiza mama huyo kichakani na kumchoma kisu tumboni na shingoni na kisha kumpora pesa shilingi milioni 2.5 na kumwacha katika hali mbaya.
Mama huyo aliokotwa na wafugaji walio kuwa wakilisha mifugo katika eneo hilo na kuwaeleza kilichompta hata hivyo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na jeshi la polisi linaendelea uchunguzi wa tukio hilo
Blogzamikoa
No comments:
Post a Comment