Friday, August 17, 2012

AMUUA MKEWE KWA SHOKA KISHA NAE AJINYONGA


Na Walter Mguluchuma, Mpanda Katavi Yetu
Mkazi wa kijiji cha Nsungwa Kata ya Ikola wilayani Mpanda mkoa wa Katavi amemuua mkewe kwa kumkata kata na shoka na kisha yeye menyewe kujinyonga baada ya kumshutumu mkewe kumuambukiza ugonjwa wa ukimwi na kuacha ujumbe wa maandishi unaomlaumu mkewe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari amewataja marehemu hao wawili ambao walikuwa wanandoa kuwa ni Alfonsi Joseph (21) na mkewe alijulikana kwa jina moja la Neema.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa nne asubuhi nyumbani kwa wanandoa hao.
Alisema siku hiyo ya tukio Alfonsi alianza kwa kumshutumu mkewe ambaye alikuwa na ujauzito kuwa amemwambukiza ugonjwa wa Ukimwi kutokana na tabia yake ya kutoka nje ya ndoa hata baada ya kumkanya mara kwa mara.
Kamanada Kidavashari alieleza katika ugomvi huo Alfonsi alizidi kumlaumu mkewe kuwa yeye ndiye aliyekuwa sio mwaminifu kwenye ndoa yao na kudai kuwa yeye mwanaume alikuwa ametulia.
Hali hiyo ya kuwa mwasirika ilimfanya kukataliwa na kila mwanamke ambaye alitaka kumuoa kwa madai kuwa ni muathirika wa Ukimwi.
Baada ya mabaishanao ya muda mrefu Neema alimweleza wazi mumewe kuwa ni mwasirika wa ugonjwa wa ukimwi na aligundua hivi karibuni baada ya kwenda Kliniki kutokana na kuwa mjamzito.
Kidavashari alieleza baada ya mkewe kukiri kuwa ameathirika ndipo mumewe alipoanza kumshambulia kwa kumkatakata  kwa shoka shingoni na kichwani hadi kufa
Baada ya kuona mkewe amefariki dunia Alfonsi aliamua kunywa maji ya betrii ya gari ili kujiua lakini aliona anachelewa kufa na kisha aliamaua kujinyonga kwa kutumia Kanga katika mti ambao ulikuwa nyumbani kwa wanandoa hao
Katika nguo alizokuwa amevaa marehemu Alfonsi kulikutwa na ujumbe wa maandishi alioandika kuwa ameamua kumuua mkewe kwa kuwa amemwambukiza Ukimwi wakati yeye alikuwa ametulia kwa kuwa mwaminifu kwa ndoa yake.
Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari kwa kufuatia tukio hili amewataka wakazi wa mkoa wa katavi kujiepusha na uasherati ili kuepukana na maradhi ya Ukimwi
Blogzamikoa

No comments:

Post a Comment