Na Walter Mguluchuma
Mpanda-Katavi yetu Blog
Mkazi wa kijiji cha Nsungwa kata ya Ikola wilayani mpanda mkoa wa Ktavi amemuua mkewe kwa kumkata kata na shoka na kisha yeye menyewe kujinyonga baada ya kumshutumu mkewe amemuambukiza ugonjwa wa ukimwi na kuacha ujumbe wa maandishi unaomraumu mkewe.
Kamanda wa polisi mkoa wa katavi Dhahiri Kidavashari amewataja marehemu hao wawili ambao walikuwa wanandoa kuwa ni Alfonsi Joseph (21) na mkewe alijulikana kwa jina moja la Neema.
Tukio hilo limetokea hapo jana majira ya saa nne asubuhi nyumbani kwa wanandoa hao.
Alisema siku hiyo ya tukio Alfonsi alianza kwa kumshujumu mkewe ambaye alikuwa na ujauzito kuwa amemwambukiza ugonjwa wa Ukimwi kutokana na tabia yake ambayo alikuwa nayo na hapo nyumba alidai alikuwa amemkanya mara nyingi.
Kamanada Kidavashari alieleza katika ugomvi huo Alfonsi alizidi kumraumu mkewe kuwa yeye ndiye aliyekuwa sio mwaminifu kwenye ndoa yao na yeye mwanaume alidai alikuwa ametulia.
Hali hiyo ya kuwa mwasirika ilimfanya yeye kla mwanamke ambaye alimuhitaji ili amuoe amekuwa akimkataa kwa kile alichokuwa akijibiwa kuwa yeye Alfonsi ni mwasirika wa ugonjwa wa Ukimwi.
Baada ya mabaishanao ya muda mrefu Neema alimweleza wazi mumew kuwa ni mwasirika wa ugonjwa wa ukimwi ambao uligunduliwa hivi karibuni alipokwenda Kriniki kwa ajili ya kupata huduma za akina mama wajawazito na ndipo walipo mpima wakamwambia kuwa ameathirika.
Kidavashari alieleza baada ya mkewe kukiri kuwa ameathirika ndipo mumewe alipoanza kumshamulia mkewe kwa kumkatakata kwa shoka shingoni na kichwani hadi kufa
Baada ya kuona mkewe amefariki dunia Alfonsi aliamua kunywa maji ya betrii ya gari ili kujiua lakini aliona anachelewa kufa na kisha aliamaua kujinyonga kwa kutumia Kanga katika mti ambao ulikuwa nyumbani kwa wanandoa hao
Katika nguo alizokuwa amevaa marehemu Alfonsi kulikutwa na ujumbe wa maandishi alioandika kuwa ameamua kumuua mkewe kwa kuwa amemwambukiza Ukimwi wakati yeye alikuwa ametulia kwa kuwa mwaminifu kwa ndoa yake.
Aliandika kibaya zaidi kilichomfanya nay eye ajiue ni kitendo cha kugundua kuwa mkewe ameathirika na kisha alipoamua kutaka kuowa mwanamke mwingine wamekuwa wakimkataa kwa kuwa eti ameathirika ndio maana nimeona bora tufe wote wawili.
Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari kwa kufuatia tukio hili amewataka wakazi wa mkoa wa katavi kujiepusha na uasherati ili kuepukana na maradhi ya Ukimwi
No comments:
Post a Comment