Na Walter Mguluchuma.
Katavi .
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Katavi katika kutekeleza majukumu yake kwa kipindi cha kuanzia julai 2017 hadi machi 2018 imepokea jumla ya malalamiko 78 ya vitendo vya rushwa na kufungua majalada 18 ya uchunguzi huku ofisi hiyo ikiwa na majalada 115 ya uchunguzi yanayoendelea kuchunguzwa .
Hayo yalisemwa hapo jana na Kaimu mkuu wa TAKUKURU wa Mkoa wa Katavi Cristophar Nakua wakati alipokuwa akisoma taarifa ya utekelezaji ya kipindi cha robo tatu ya mwaka kwa Wandishi wa habari wa vyombo mbalimbali ofisini kwake .
Alisema Taasisisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa ni moja ya Taasisi za Serikali inayotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na kuandaa taarifa za utendaji kazi ya kila mwezi ,robo mwaka ,nusu na mwaka mzima kwa ajiri kujipima kulingana na mpango mkakati wa Taasisi hiyo.
Alifafanua kuwa taarifa zilizopokelewa zimeanisha idara Taasisi mbalimbali zilizotuhumiwa na vitendo vya rushwa ikiwa ni Taasisi za Serikali na binafsi ambapo Halmashauri kimkoa zina jumla ya malalamiko 78,polisi 6 chama cha ushirika 2 sekta binafsi 2 na siasa mawili uhamiaji moja .
Mengine ni malalamiko ni upande wa Serikali ya vijiji malamiko 10, baraza la ardhi na nyumba Wilaya moja ,Baraza la kata , Tanesco , uhamiaji ,0fisi ya makazi ya wakimbizi na sekta ya madini .
Nakua alieleza kuwa TAKUKURU Mkoa wa Katavi inajumala ya kesi 13 zinazoendelea Mahakamani zikiwa katika hatua mbalimbali huku kesi sita zikiwa ni kesi mpya .
Katika kuelimisha umma makundi mbalimbali yamefikiwa kukiwa na lengo ya kuyaongezea makundi hayo ufahamu wa kutosha wa masuala ya rushwa ili yawe na ufahamu wa kutosha wa maswala ya rushwa ili yawe mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya rushwa .
TAKUKURU Mkoa wa Katavi imefanikiwa kuokoa TSHS 3 ,045,000 ambazo ni marejesho ya mshahara uliolipwa kwa mtumishi aliyekuwa amefariki ambae alikuwa ni mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele.
Nakua alisema pIA wameweza kufanya kazi ya ufuatiliaji wa fedha za miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele ambapo jumla ya fedha za miradi yenye thamani ya Tshs 3,806 380,694. Imefanyiwa ufuatiliaji na TAKUKURU Mkoa wa Katavi.
MWISHO
No comments:
Post a Comment