Na Walter Mguluchuma .
Katavi
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii TASAF katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi imeanzisha utaratibu mpya wa kuwalipa walengwa wa MFUKO Kaya maskini kwa njia ya mtandao na kuwafungulia akaunti Benki bure.
Afisa ufuatiliaji wa TASAF wa Manispaa ya Mpanda Twambulile Solomon alisema utaratibu huo mpya wa kuwalipa walengwa wa mfuko huo katika Mkoa wa Katavi ulianza mwezi julai mwaka jana katika Manispaa ya Mpanda .
Utaratibu huo mpya kwa hapa nchini umeanza katika Halmashauri 16 kwa ajiri ya majaribio na kwa Mkoa wa Katavi utaratibu huo unafanyika katika Manispaa ya Mpanda huku lengo likiwa ni kutaka utaratibu huo wa malipo kwa njia ya mtandao ufanyike katika Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi .
Twambulile alisema kwa kipindi cha kuanzia Julai mwaka jana hadi sasa wameisha walipa walengwa malipo yao kwa njia ya mtandao kiasi cha Tshs Milioni 67,459,500 .
Alifafanua kuwa hadi kufikia mwezi wa pili mwaka huu dilisha lilikuwa linawalipa walengwa 344 kwa njia ya mtandao ambapo kwa kipindi cha mwezi machi na aprili walengwe wengine 300 wamejiunga na utaratibu huo wa kulipwa kwa njia ya mtandao .
Afisa ufuatiliaji huyo wa Tasaf alisema kwa kipindi cha mwezi Aprili wameweza kuwafungulia walengwa 71 akaunti katika Benki ya CRDB Tawi la Mpanda bila malipo yoyote yale na akaunti zao hazitakuwa na makato yoyote yatakayo katwa kwenye akaunti zao
Alizitaja mitaa ambazo walengwa waliofunguliwa akauti Benki kuwa ni Kawajense walengwa wa dirisha 30 Kamakuka walengwa 14, Mbugani Kakese walengwa walengwa 24 na Kijiji cha Mwamkulu walengwa 4.
Kwa upande wake mmoja wa walengwa hao Salome John alisema kuwa utaratibu huo utawazidi kuwahakikishia usalama zaidi wa fedha zao kuliko ilivyokuwa awali na utawapunguzia usumbufu wa kupanga foleni kwenye malipo.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kawajense Simon Jumapili alisema utaratibu huo wa walipo kwa njia ya mtandao utawasaidia walengwa kwenda kuchukua fedha zao kwa muda wanaotaka wao tofauti na hapo awali walipokuwa wakipangiwa muda wa kwenda kuchukua fedha zao.
Pia utawafanya walengwa wa mfuko kwenda kuchukua fedha zao pindi wanapokuwa wamemaliza shughuli zao za nyumbani .
No comments:
Post a Comment