Na Walter Mguluchuma.
Serikali imetowa tamko kuwa haina mpango wa kutowa fedha za mikopo kwa wachimbaji wadogo bali watatoa mkopo wa vifaa baada ya kubaini fedha zilizokuwa zikitolewa kwa wachimbaji wadogo zilikuwa hazitumiki ilivyokusudiwa.
Kauli hiyo ya Serikali ilitolewa hapo jana na Naibi Waziri wa Madini Doto Biteko wakati alipokuwa akiwahutubia wachimbaji wadogo wa madini wa Mkoa wa Katavi katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika machimbo ya dhahabu ya Ibindi Wilayani Mpanda .
Alisema Wizara ya madini imeondoa utaratibu wa hapo awali wa kuwakopesha fedha wachimbaji wadogo kwa ajiri ya kununulia vifaa vya kufanyia shughuli za uchimbaji na badala yake watakuwa wanawakopesha vifaa na sio fedha tena .
Wamebaini kuwa fedha zilizokuwa zikitolewa na Serikali kwa ajiri ya kuwakopesha wachimbaji wadogo zimekuwa hazitumiki kama ilivyokusudiwa na badala yake wamekuwa wakizitumia kwa matumizi mengine .
Alieleza wachimbaji wadogo wamekuwa wakikopeshwa fedha kati ya Tshs Milioni 100 na milioni 200 lakini wachimbaji badala ya kununua vifaa vya kuchimbia madini wao wao wamekuwa wakizitumia kwa ajiri ya kununua magari na kujengea nyumba .
Alisisitiza kuwa wachimbaji wadogo wote walikopeshwa fedha na wakashindwa kuzirudisha wanatakiwa wazirudishe mara moja kwani kwa wale watakao shindwa kurejesha wakakamatwa na kufikishwa mahakamani .
Aliwataka wachimbaji wote wa madini hapa nchini wawe waaminifu kwenye kulipa kodi za Serikali na wachimbaji wadogo waache tabia yao ya vichochoro vya kusafirisha madini kwa njia ya magendo kwani mchango wa sekta ya madini bado ni mdogo kwenye mapato ya Taifa kutoka na madini mengi kuzushwa nje ya nchi .
Alisema Serikali haiko tayari kuona kazi zinazoweza kufanywa na Wanzania kwenye migodi ya madini zinafanywa na watu wa kutoka nchi za nje kwani lengo la Serikali ni kutaka kuona Watanzania wananufaika na rasilimali za madini .
Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wadogo wa Mkoa wa Katavi Willy Mbogo aliiomba Wizara ya madini kutunga sheria ambazo zitakuwa zinawapa nafuu kwani sheria za sasa haziangalia aina ya wachimbaji wadogo na wakubwa .
Alisema yapo maeneo ambayo ambayo baadhi ya wachimbaji wanayamiliki kwa kuwa na leseni lakini yamekuwa hayaendelezwi hivyo ni vema serikali ikawafutia leseni wachimbaji hao .
Katibu wa chama wa wachimbaji wadogo wa Mkoa huu Filberti Sanga aliomba wizara ya madini iwafutie leseni wachimbaji ambao wachindwa kuyaendeleza na bbadala yake wapewe wachimbaji wadogo .
Alisema wapo wamiliki wa leseni za madini ambao maeneo yao hawayaendelezi wamekuwa wakibadili majina kila muda wao wa leseni kumalizika kwa kuhofia kufutiwa leseni zao .
MWISHO
No comments:
Post a Comment