Kamanda Damas Nyanda akionyesha gobore lillokamatwa na jeshi
la polisi kufuatia msako waliofanya jana huko katika Kijiji cha
Ugalla Wilaya ya Mpanda .
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda akionyesha
vipande vya meno ya waliokamatwa nayo watuhumiwa waliokamatwa
wakiwa na silaha tatu za kivita story imeisha tangulia
Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Watu watatu kati ya watuhumiwa watano wanashikiliwa na jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi baada ya kukamatwa wakiwa na silaha nzito tatu na magazine tano risasi 16 na vipande vinne vya mame ya tembo yenye thamani ya zaidi ya TSHS 34 baada ya mabishano ya risasi baina yao na Askari Polisi na Wahifadi ya Taifa ya Katavi huku watuhumiwa wawili wakiuawa katika tukio hilo .
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mbele ya Wandishi wa Habari hapo jana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda alisema tukio hilo hilo la kamatwa kwa wathumiwa hao watatu na wawili kuuawa lilitokea hapo juzi majira ya saa sita usiku huko katika Kijiji cha Kapalamsenga Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi .
Alisema watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia msako mkali uliofanywa kwa muda wa wiki tatu na Jeshi la Polisi na Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi ambao walipata taarifa juu ya watu hao kujihusisha na maswala ya ujambazi na ujangili ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi .
Baada ya kuwa wamepata taarifa hizo ndipo walipo fanya msako huu uluodumu kwa muda wa wiki tatu za kuwasaka watuhumiwa hao ulikuwa ukifanyika usiku na mchana .
Kamanda nyanda alieleza ndipo hapo juzi Askari hao walipofanikiwa kuwakamata watuhimiwa hao baada ya mabishano makali ya kurushiana risasi ambapo katika tukio hilo watuhumiwa wawili kati ya watano waliweza kuuawa kwa kupigwa risasi .
Alisema baada ya kutiwa nguvuni watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na bunduki tatu za kivita aina ya SMG ,risasi 16, magazine tano na vipande vinne vya meno vyenye uzito wa kilo 6.6 yenye thamani ya Tshs 34,050,000.
Pia watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na nyama ya pofu kilo 20 zenye thamani ya Tshs 3,859,000 wakiwa wamehiifadhi ndani ya mfuko wa sandarusi .
Kamanda Nyanda alisema watuhumiwa hao wanaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi na wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi utakapo kuwa umekamilika .
Kamanda Nyanda ametowa wito kwa watu waheshimu sheria na waache kufanya uhalifu kwani maisha ya uhalifu ni mafupi na amewataka wananchi wanapokuwa wameona viashiria vya uharifu watowe taarifa kwenye vyombo husika .
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi Izumbe Msindai alisema ushirikiano wa Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi na Polisi ndio umefanya watuhumiwa hao kukamatwa .
Alisema Hifadhi ya Katavi wataendelea kushirikiana na wananchi wanao zunguka hifadhi hiyo katika kukabiliana na swala zima la ujangili wa wanyama ndani ya Hifadhi na nje ya Hifadhi.
No comments:
Post a Comment