Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Mashekh watano kati ya sita wanaunda baraza la Halmashauri ya Bawata ya Mkoa wa Katavi wametangaza kujiuzuru nafasi hiyo kwa kile walichodai kuwepo kwa mingongano ya uongozi na ukiukwaji wa katiba ya Bakwata .
Mashehke hao walitangaza hatua yao ya kuziuzu hapo jana katika kikao chao na wandishi wa habari kilichofanyika hapo jana mjini hapa na kuhudhuriliwa na Mwenyekiti wao Shekh shaban Bakari .
Waliotangaza kujiuzuru ni Shekhe Mashaka Nassoro Kakulukulu, Shekhe Hassani Mbaruku, Said Hruna Omary , Mohamed Shabani Sigulu na Mwenyekiti wao wa baraza la Halmashauri ya Bakwata Mkoa wa Katavi .
Kwa upande wake Shekhe Mashaka Nassoro Kakulukulu alisema yeye haoni sababu ya kuendelea na nafasi hiyo kwa kile alichodai kuwa kumekuwepo na baadhi ya mambo ya kimaendeleo yemekuwa hayaendi sawa ndani ya uongozi wa Bakwata Mkoa wa Katavi .
Alisema kuwa hata katiba ya Bakwata imekuwa ikikiukwa na kumekuwepo na mgongano wa baadhi ya maamuzi yanayotolewa na vikao halali vya kuleta maendeleo na kutenguliwa na vikao visivyo halali kwa mujibu wa katiba ya Bakwata .
Shekhe Said Omary alisema yeye sababu kubwa ilimfanya achukue uamuzi huo wa kujiuzuru ni kutokana na mazingira ya viongozi wa Bakwata kutofuata Katiba .
Mohamed Shaban Sigulu alisema yeye ameamua kujiuuzuru kutokana na uongozi wa Bakwata kuwa na msuguano hari ambayo imefanya hata miradi ilipo kusimama kutokana na msuguano wa kiuongozi .
Alifafanua kuwa msuguano huo uliopo ndani ya Bakwata umesababisha hadi mwalimu wa madras I katika msikiti mkuu wa Mkoa wa Katavi kuamua kuacha kazi hiyo hivi karibuni.
Mwenyekiti wa Baraza la Halmashauri ya Bakwata wa Mkoa Shaban Bakari alisema ameamua kujiuzuru nafasi hiyo kwa ajiri ya kuwepo kwa msuguano ndani ya uongozi wa Bakwata Mkoa hari ambayo imekuwa ikisababisha baadhi ya vikao kufanyika bila kuwepo kwa wajumbe halali wa vikao husika .
Hivyo yeye haoni tena sababu ya yeye kuendelea kuwa Mwenyekiti na badala yake anaona ni vema watafute mtu mwingine afanye kazi hiyo.
No comments:
Post a Comment