Na Walter Mguluchuma
Katavi .
Meya wa Manispa ya Mpanda Willy Mbogo amekanusha vikali taarifa ambazo ambazo vimeenea katika maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Katavi za kuwa yeye anao mpango wa kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu ujao wakati jambo hilo halina ukweli wowote kwani yeye hana mpango wa kugombea ubunge kwenye jimbo lolote la Mkoa wa Katavi
Mbogo ambae ni Diwani wa Kata ya Kashauli CCM alitowa kauli hiyo jana wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Kata ya Majengo wakati wa uzinduzi wa kisima cha maji kilichojengwa na Kampuni ya kuuza mafuta ya GBP kilichogharimu kiasi cha shilingi Milioni 55 ikiwa ni msaada uliotolewa na Kampuni hiyo .
Alisema yeye amekuwa akizushiwa kuwa anao mpango wa kugombea ubunge katika Jimbo la Mpanda Mjini jimbo ambalo linaongozwa kwa sasa na Sebastiani Kapufi .
Alisema kuwa napenda kuwahakikishia wakazi wa Manispaa ya Mpanda na wananchi wa Mkoa wa Katavi kwa ujumla wake kuwa yeye hana mpango wa kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu ujao wa 2020 kwenye jimbo lolote la Mkoa wa Katavi.
Alifafanua kuwa nafasi ya udiwani aliyonayo inamtosha sana hivyo ataendelea kuwatumikia wananchi kwa nafasi hiyo ya udiwani kwani inamfanya kila siku kufanya kazi ya kuwatumika wananchi kwa karibu zaidi.
Nimekuwa nikuzushiwa mara kwa mara kuwa anampango wa kugombea udiwani na hata hivi karibuni wakati wa mkutano mkuu wa CCM wa Wilaya ya Mpanda baadhi ya wajumbe wa mkutano huo walihoji swala hilo alisema Mbogo .
Alisema ameamua kukanusha swala hilo mapema kwani anaona siku hadi siku watu wanaendelea kuzusha swala hilo ambalo yeye wala haliko hata moyoni mwake kwa sasa wala wala hakilii kabisa zaidi ya kuwaendelea kuwatumukia wananchi wake kwa nafasi ya udiwani.
Alieleza kuwa wakati wa mkutano Mkuu wa uchaguzi uliofanyika yeye aligombea ujumbe wa mkutano mkuu wa Taifa na aliweza kushinda nafasi hiyo licha ya watu ambao walikuwa wameanza kumzushia kuwa kwanini agombee nafasi hiyo wakati pia anampango wa kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu ujao .
MWISHO
No comments:
Post a Comment