Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma.
Katavi
WAZAZI wa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 12 ambae ni mlemavu wa kusikia na kusema ‘bubu kiziwi “ wanadaiwa kumuozesha kwa nguvu kwa kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 18 imeinika .
Wazazi hao na wanandoa hao wote wanaishi katika kijiji cha Masigo kilichopo katika wilaya ya Mlele mkoani Katavi .
Mratibu wa Marie Stopes mkoa wa Katavi , Seif Kajiko amelaani kitendo hicho chs wazazi hao kumuozesha mtoto wao huyo wa kike kwa nguvu akidai kunasababishsa kuongezeka kwa mimba za utotoni mkoani humo .
Kajiko alilaani tabia hiyo wakati wa maadhimisho ya tamasha la vijana lililojumiisha wanafunzi kutoka shule kumi za sekondari za Manispaa ya Mpanda lililoandaliwa na Marie Stopes kwa
kushirikiana na Ofisi ya Mganga Mkuu wa mkoa wa Katavi ambapo
yalifanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili mjini hapa .
Aliiasa jamii mkoani humo kuachana na tabia hiyo ya kuwaozesha binti zao wenye umri mdogo kwa kuwa madhara yake ni makubwa ikiwemo vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na matatizo ya uzazi .
Alisisitiza kuwa pamoja na jitihada zinazofanywa na Marie Stopes kukabiliana na mimba za utotoni kwa kutoa elimu shuleni bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya waliku wa shule za sekondari kukataa kutolewa kwa elimu ya uzazi wa mpango kwa wanafunzi wa kike .
Kwa upande wake Mratribu wa Vijana wa Marie Stopes nchini , Daniel Mjema lengo la tamasha hilo ni kutoa elimu ya afya ya msingi kwa vijana elimu ya uzazi wa mpango na jinsi ya kujikinga na maabukizi ya VVU na Ukimwi .
Nae Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Katavi , Wilbroad Marandu aliwaasa wanaume wote moani humo kushirikiana bega kwa began a wenza wao na kujitokeza kupata elimu ya uzazi wa mpango .
“Baadhi ya wanaume wana tabia ya kuwazuia wake zao kujiunga na uzazi wa mpango kwa kisingizio kuwa mwanamke ni wa kuzaa tu hadi mayai yake ya uzazi ya muishie “ alisisitiza
Kwa
upande wake Mwanafunzi wa Shule ya Sekinari ya Wasichana Mpanda alidai
kuwa mimba na ndoa za za utotoni zinamkwamisha mtoto wa kike kutimiza
ndoto zake .
Mwisho
No comments:
Post a Comment