Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii Jinsia , Wazee na Watoto inatarajia kutowa ajira kwa watumishi wa kada mbalimbali za afya na watakao pewa kipaumbele cha kwanza katika ajira hizo ni wale wakatao omba kufanya kazi katika Mikoa ya pembezoni ambayo inaupungufu mkubwa wa watumishi wa Afya.
Kauli hiyo ya Wizara ya Afya ilitolewa hapo jana na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati alipokuwa akiwahutubia wakazi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katav katika uwanja wa mpira wa Polisi Mpanda alipokuwa akifungua upimaji na utoaji tiba wa magonjwa yasiyo ambukiza .
Waziri Ummy Mwalimu alieleza kuwa Serikali inatarajia kutangaza ajira za watumishi 52,000 wa kada mbalimbali hivi karibuni hivyo kwa nafasi za ajira zitakazo tolewa na Serikali kwa ajiri ya Wizara yake watatowa kipaumbele kwa Mikoa tisa ambayo inaupungufu mkubwa wa watumishi wa Afya .
Alisema kwa wale ambao watakao omba kupangiwa kufanya kazi katika Mkoa wa Dares salaam hawata kuwa na nafasi ya kuchaguliwa kwanza kwani Mkoa huo hauna tatizo kubwa kama ilivyo Mikoa ya pembezoni .
Aliitaja baadhi ya Mikoa yenye upungufu mkubwa wa watumishi wa kada ya Afya na ambayo itapewa kipaumbele ili kupunguza tatizo la watumishi kwenye Mikoa hiyo kuwa ni Mikoa ya Katavi ,Rukwa ,Kigoma, Simiyu, Shinyanga , Tabora Geita na Kagera.
Waziri Mwalimu pia alieleza kuwa Wizara ya yake imeandaa mpango wa kupeleka Bungeni mswada wa kumtaka kila mtu iwe ni lazima kujiunga na mfuko wa Bima ya afya
Aliwaonya watumishi wa Wizara hiyo ambao wanatabia ya kuchezea fedha za kununulia dawa na aliwataka waache mara moja na kwa wle watakao bainika watachukuliwa hatua kali .
Nae Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga alieleza kuwa Mkoa wa Katavi unajumla ya Watumishi 692 kati ya watumishi 2,174 wanaohitajika kati yao 17 ni watumishi wa ngazi ya Mkoa na 675 ni wangazi ya Serikali za Mitaa.
Alifafanua kuwa Mkoa wa Katavi unajumla ya upungufu wa watumishi 1,186 sawa na asilimia 69 ya mahitaji ya watumishi.
Kwa mwaka wa fedha wa 2016 na 2017 Mkoa na Halmashauri zake tano umeidhinisha kuajiri jumla ya watumishi wapya wa kada mbalimbali za Afya wapatao 422.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Katavi Anna Shumbi alieleza kuwa Mkoa huo ni miongoni mwa Mikoa hapa nchini unaoongoza kwa mimba za utotoni .
Alieleza sababu zinazochangia Mkoa huo kuwa na mimba nyingi za utotoni kuwa zimekuwa zikisababishwa na wazazi kuwaacha watoto wao peke yao bila kuwa na uangalizi hasa kipindi cha masika ambapo wazazi uhamia mashambani na kuwaacha watoto peke yao .
MWISHO
No comments:
Post a Comment