Walter Mguluchuma Na Arine Temu
Katavi yetu Blog
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imetowa mafunzo kwa wandishi wa Habari wa Mkoa wa Katavi ya utumiaji wa huduma za Mawasiliano ya huduma ya kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu ya kiganjani .
Mafunzo hayo ya siku moja yaliowashirikisha Wandishi wa Habari wa vyombo mbali mbali vya Habari vilivyopo katika Mkoa wa Katavi yalifanyika katika ukumbi wa Hotel ya Lyamba lyamfipa Mjini hapa .
Mwandisi Mwandamizi wa mawawasiliano wa TCRA wa wa Kanda ya Nyanda za juu kusini Eng FelicianMwesigwa alisema MNP ni huduma ya hiari inayompa mtu uhuru na kumwezesha kuhamia mtandao wowote anao utaka na kuendelea kupata mawasiliano bila kulazimika kubadili namba yake ya simu .
Huduma hiyo inaongeza ushindani kwenye sekta ya mawasiliano na hivyo kuwa ni kichocheo cha utoaji wa huduma bora na zenye gharama nafuu kwa maana kama mtu ataona huduma haziridhishi basi wateja watahama na kuhamia kwenye mtandao mwingine .
Eng Mwesigwa alisema huduma ya kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba yako itamwezesha mteja kubaki na namba yake ya awali anapo hama kwa mtoa huduma moja kwenda nyingine.
Alisema huduma hiyo inaokoa gharama ya fedha kwa mteja kwa kuwa hatakuwa na haja ya kununua laini mpya kwa kila mtoa huduma au kuwa na simu ya kiganjani zaidi ya moja ikiwa lengo ni kubaki na namba zako .
Nae Naibu Mkurugenzi anaeshughulikia masuala ya watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano Thadayo Ringo alieleza mfumo wa kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu ya kiganjani utatumiwa na wateja wote nchini wanaolipia huduma kwanza na wanaolipia huduma baada ya matumizi.
Ili kuingia kwenye mfumo huu simu ya mtumiaji lazima iwe inatumika yaani haijafungiwa au kusimamishwa kwa muda na huwezi kuhama na salio lililopo na unatakiwa kutumia salio kabla ya kuhama la sivyo salio lako litatunzwa katika akaunti maalumu ya mtoa huduma wako wa zamani na utalazimika kufuata taratibu za kudai ili urudishiwe.
No comments:
Post a Comment