Na Walter Mguluchuma..
Katavi .
Wizara ya Maliasili na Utalii imewataka wadau wa uhifadhi kuunga mkono mpango wa Rais Dk Pombe Magufuli wa kujenga mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme STIGO katika Mto Rufiji ndani ya pori la akiba Selou ambao utazalisha zaidi ya Negawati 2,100 za umeme kama hatua muhimu ya ya kusaidia maendeleo ya Nchi kuelekea Tanzania ya viwanda.
Wito huo ulitolewa naKatibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Generali Daudence Milanzi wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya askari wa wanyama pori kutoka Mamlaka ya Wanyama pori Tanzania TAWA na Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro yaliofanyika katika kituo cha mafunzo Mlele Mkoani Katavi .
Alisema kwa kutambua umuhimu wa uhifadhi Tanzania imetenga eneo la asilimia 28 ya eneo lote la Nchi kavu Tanzania Bara kwa ajiri ya uhifadhi wa wanyama pori na mistu ikiwemo vyanzo vya maji ambapo uhifadhi lazima uwe kwa manufaa ya Watanzania na maendeleo kwa Taifa .
Meja Generali Milanzi alieleza kuwa dhamira ya Serikali kujenga mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa STIGULAS GORCE ndani ya pori la akiba na ujenzi wa mradi wa maji wa bwawa la Kidunda utachukua eneo dogo la pori hilo .
Alifafanua kuwa pori hilo linaukubwa wa zaidi ya kilometa za mraba elfu 50 ambazo ni zaidi ya ukubwa wa Nchi za Rwanda na Burundi zikiunganishwa pamoja
Pia alisema hivi sasa uhifadhi unakabiliwa na tatizo la uvamizi wa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi hivyo Wizara inatowa wito kwa wahifadhi kushirikiana na mamlaka za Mikoa na Wilaya kwenye maeneo yao.
Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya wanyama pori Tanzania TAWA Martin Loibook aliwashukuru wadau wa uhifadhi wa ndani na nje ya Nchi ambao wanaendelea kufadhili mafunzo ya askari na vitendea kazi ili kuimarisha ulinzi na uhifadhi wa wanyama pori . na kukabiliana na ujangili ukiwemo wa Tembo
Alisema Tembo wameanza kuongezeka kwenye maeneo mbalimbali Nchini baada ya kufanyika kwa doria nyingi ambazo zimefanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa wengi na silaha walizokuwa wakizitumia kufanyia ujangili .
Nao baadhi ya wadau wa uhifadhi wamezungumzia umuhimu wa mafunzo yanayoendelea kutolewa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa askari na watumishi wa Wizara hiyo kuwa yanalenga kuwa na mfumo wa Jeshi Usu katika ulinzi wa usimamizi wa maliasili za Taifa .
No comments:
Post a Comment