Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Madiwani wa Manispaa ya Mpanda katika Mkoa wa Katavi kwa kauli moja wametowa tamko la kumpongeza Rais John Magufuli kwa hatua muhimu anazozichukua za kuhakikisha Watanzania wanafaidika na kunufaika na rasilimali zilizopo za Nchi .
Pongezi hizo za Madiwani wote 21 wanaounda Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Mpanda zilitolewa hapo jana mbele ya wandishi wa Habari Mjini hapa wakati walipokuwa wakitowa tamko hilo kwa Wandishi wa Habari .
Akitowa tamko la pongezi hizo Meya wa Manispaa Willy Mbogo alisema Madiwani wote wa Manispaa ya Mpanda kwa kauli moja wanampongeza sana Rais John Magufuli kwa hatua muhimu za kijasiri anazochukua za kuhakikisha Watanzania wananufaika na kufaidika na rasilamali alizowapatia Mungu na wanamuunga mkono kwa asilimia miamoja .
Alisema ujasiri , uthubutu na utayari aliouonyesha Rais Magufuli kwa faida ya Watanzania ni wakiwango cha juu kwa binadamu wa kawaida na wanaipongeza pia kamati zote mbili zilizoibua mambo mengi ambayo Watanzania walikuwa hawayafahamu .
Wanashangaa na kulaani vikali kwa mtu yoyote ambaye atatumwa na kuhongwa na Mabeberu ili adhoofishe vita hii ya kiuchumi huyo ni msaliti wa Taifa letu na anapaswa kulaniwa na kuzomewa na Watanzania wote .
Mbogo alieleza kuwa tutambue juhudi hizi za Rais wetu mwisho wake ni faida kubwa kwetu sote Watanzania ,Serikali yetu na Halmashauri zetu kwani Nchi itaongeza mapato yake .
Aliwaomba Wabunge wote waondoe itikadi zao za vyama na wawe pamoja kwenye vita hii na kila wakati kwenye jambo lolote ambalo lenye masilahi kwa Taifa ..
Alifafanua jambo kama linamasilahi ya Taifa hata kama linasemwa na mtu wa mpinzani liungwe mkono na kama linasemwa na mtu wa chama tawala lenye masilahi ya Taifa basi liungwe mkono na hata wapinzani .
Aidha IMadiwani wanawalani vikali sana wale wote ambao wamekuwa wakituibia na kupola mapato ya Watanzania kupitia rasilimali za madini yetu .
Diwani wa Kata ya Makanyagio Haidari Sumry alisema juhudi hizo zinazofanywa na Rais ni mkombozi kwa Halmashauri zote hapa nchini kwani zitaongeza kipato chao .
Nae Diwani wa Viti maalumu Jojina Kisalala aiwataka wnawake wote wamuunge mkono Rais wetu kwa kuibua mambo mengine mengi ambayo bado yamefichika .
Alisema Magufuli amewek a historia kwa kuthibiti rasilimali za Nchi ambazo zilikuwa zikitoroshwa nje ya Nchi na kuikosesha Serikali y etu mapato .
MWISHO
No comments:
Post a Comment