Walter Mguluchuma Na Arine Temu
Nkasi
KUTOKANA na kutojua umuhimu wa elimu kwa baadhi ya
watoto wa kike wilayani Nkasi mkoani Rukwa kumesababisha baadhi ya
watoto wa kike waliopewa fursa maalumu ya kulipiwa mafunzo ya ufundi wa
aina mbalimbali ikiwemo ujasiliamali na makenika na shirika la Plan
International, wameacha mafunzo hayo na kudai kuwa wao ni warembo na
hawafai kusomea ufundi makenika.
Hayo yamebainishwa jana na Nestory
Frank mratibu wa ndoa za utotoni kutoka shirika la Plan International
wilayani Nkasi Katika mafunzo ya siku mbili inayofanyika katika ukumbi
wa Mtakatifu Bakita na kuwakutanisha wajumbe wa kamati ya wilaya ya
kumlinda mtoto wa kike dhidi ya mimba za utotoni.
Alisema
kuwa shirika hilo liliandaa program maalumu ya kuwapatia mafunzo watoto
wa kike waliopata ujauzito katika umri mdogo kutoka kata tatu za
Mtenga, Mkwamba na Nkandasi ili waweze kupata mafunzo hayo
yatakayowasaidia kujikomboa ki uchumi baada ya kufuzu mafunzo hayo na
kuanza kufanya shughuli za uzalishaji Mali kwa faida zao.
Frank
alisema kuwa baadhi ya watoto hao wakike wameamua kuacha kuhudhuria
mafunzo hayo wakidai kuwa hawataki kusomea baadhi ya kozi huku wengine
wakiwa walikatisha masomo na hawajui kusoma na kuandika lakini
wanang'ang'ania kusomea fani ambazo zinahitaji elimu kubwa kitu ambacho
kimekuwa ni changamoto.
Alisema
kuwa baadhi ya watoto hao wa kike wanataka kusomea ufundi umeme ambao
unahitaji elimu kubwa lakini wakishauriwa wajifunze makenika wanakataa
wakidai kuwa wao ni warembo na hawawezi kusomea Kazi kama hiyo.
Mratibu
huyo wa ndoa za kutotoni alisema kuwa baadhi ya watoto hao wa kike
wamekuwa na masharti magumu wakidai kuwa hawapo tayari kusomea baadhi
ya mafunzo kama ufundi cherehani mpaka wanunuliwe cherehani na shirika
la Plan International ambalo linawalipia mafunzo hayo na wakabidhiwe
ziwe Mali yao ndipo wakubali kusomea mafunzo hayo.
Alisema
kuwa kuna madarasa yalikuwa na wanafunzi 25 na wameacha hadi kubakia
wanafunzi wanne wengine bila kutoa sababu hali ambayo inakatisha tamaa
kwani lengo la shirika hilo ni kuwasaidia wao waweze kujikomboa ki
uchumi kwani baadhi yao walikatishwa masomo na hawana ujuzi wowote
utakao wasaidia maishani ili wajikomboe kwa kujiajiri na kuajiliwa.
Frank
alisema kuwa changamoto nyingine ni kuwa baadhi yao wameonekana kupata
ujauzito wakiwa wanaendelea na mafunzo hayo na kulazimika kuacha
kuhudhuria wakidai kuwa wanalea mimba hivyo hawapo tayari kuendelea na
mafunzo.
Alisema
kuwa shirika la Plan International kupitia program hiyo inamlipia kila
mtoto hadi shilingi 150,000 lakini wanaamua kuacha na kurejea mtaani na
kuonekana kuwa hawahitaji kabisa mafunzo hayo na hivyo kusababisha
fedha hizo kupotea kwa kuwalipia watu wasiotaka kupata ujuzi.
Bado
wamekuwa wakiendelea kuwabembeleza ili warejee na kupata mafunzo hayo
lakini baadhi yao wamekuwa hawataki kabisa na kuacha hali ambayo
inasababisha changamoto kubwa katika utekelezaji wa mradi huo ambao
unania ya kuwasaidia wao wenyewe.
Akizungumza
katika mafunzo hayo mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Josepha Josefu
alisema kuwa miongoni mwa matatizo ni wanawake ambao mama zao na watoto
hao wakike nao wanaridhika kuona watoto wao hao wakiacha mafunzo na
wao wanaridhika inawezekana kwa kuwa nao hawajui umuhimu wa elimu.
Alisema
watoto hao ambao wanapewa ujauzito hawaolewi na matokeao yake
wanabaki nyumbani kwao wakiwalea watoto wao kwa shida na kusababisha
mzigo katika familia kwani inabidi wazazi wa mwanamke ndiyo wachukue
jukumu la kuwalea watoto wao na wajukuu na hivyo kusababisha hali ngumu
katika familia kwani wazazi wao wanabeba mizigo ambayo hawakustahili.
Josefu
alisema kuwa inatia aibu kuona mtoto wa kike aliyekatishwa ndoto zake
kwa kupewa mimba katika umri mdogo lakini amepata fursa ya kupata
mafunzo kwa kulipiwa na shirika la Plan International akiacha na wazazi
hususani mama anaridhika na kuona ni kawaida kitu kinachoumiza na
kusikitisha.
Alisema
kuwa program hiyo ni ya muda tu na itakapo malizika itawaacha katika
umasikini kwani wameshindwa kuitumia vizuri na hata watoto waliozaa
watakuwa masikini kwa kuwa wazazi wao watashindwa kuwa lea vizuri
kutokana na umasikini na kama mikoa mingine wangeipata fursa hiyo Wang
rich an gamma ili iwaokoe watoto hao wakike.
Mwisho
No comments:
Post a Comment