Walter Mguluchuma
Na Arine Temu
Katavi
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na Halmashauri ya Wilaya Mpanda katika Mkoa wa Katavi kwa kipindi cha kuanzia Julai 2016 hadi Machi 2017 zimeongoza kati ya Halmashauri zote zilizopo katika Mkoa huu kwa malamiko yanayo husiana na Rushwa .
Hayo yalisemwa hapo jana na Kaimu Mkuu wa TAKUKURU wa Mkoa wa Katavi Cristophar Nakua alikuwa akitowa taarifa mbele ya wandishi wa Habari ofisini kwake ya utekelezaji wa shughuli zao za kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2016 hadi Machi 2017.
Alisema katika kutekeleza majukumu yake TAKUKURU Mkoa wa Katavi kwa kipindi cha kuanzia Julai 2016 hadi Machi 2017 imepokea malalamiko ya vitendo vya rushwa 83 na kufungua majalada 28 ya uchunguzi ,huku ofisi hiyo ikiwa na jumla ya jumla ya majalada ya uchunguzi 118 yanayoendelea na uchunguzi .
Nakua alieleza kuwa wakati huo huo taarifa nyingine zinaendelea kufanyiwa kazi na zipo katika hatua mbalimbali na katika chunguzi zilizofanyika na zinazoendelea TAKUKURU Mkoa wa Katavi imefanikiwa kuokoa kiasi cha TSHS 10,425,000.
Alifafanua kuwa taarifa zilizopokelewa zimebainisha Wizara mbalimbali zinazotuhumiwa na vitendo vya Rushwa iiwa ni taasisi za Serikali na Sekta binafsi huku Wizara inayoongoza kwa malalamiko mengi ni TAMISEMI yenye malalamiko 68 Wizara ya Mambo ya ndani sita , Wizara ya Katiba na Sheria manne, Wizara ya Nishati na Madini mawili Wizara ya Fedha lalamiko moja na Sekta Binafsi mawili .
Kaimu Mkuu huyo wa TAKUKURU Mkoa wa Katavi alisema katika tathimini iliyofanyika katika kipindi hicho inaonyesha kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ndio zinaongoza kwa kuwa na malalamiko 25 kila moja ikifuatiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo yenye malalamiko 11, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele malalamiko 4 na Halmashauri ya Mpimbwe yenye malalamiko matatu .
Alisema TAKUKURU wataendele kutowa elimu kwa njia mbalimbali ya kuielimisha jamii juu ya madhara ya kutowa na kupokea rushwa.
mwisho
No comments:
Post a Comment