Walter Mguluchuma Na Arine Temu
Katavi .
Mwachimbaji wadogo wadogo wa madini ya dhahabu katika Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi wamemwomba Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Liliani Matinga awarusu waendelee kuchimba madini ya dhahabu katika Machimbo ya Isumamilomo ambayo yamefungwa hivi karibuni na Mkuu huyo wa Wilaya .
Wakizungumza mbele ya wandishi wa Habari hapo jana wachimbaji hao walieleza kuwa wachimbo hayo yalikuwa ndio mkombozi kwa maisha yao kutokana na riziki waliokuwa wakiipata kutoka kwenye machimbo hayo .
Mmoja wa wachimbaji hao Richald Nzingula alisema wao kama wachimbaji wanamwomba Mkuu wa Wilaya ya Mpanda awafungulie machimbo hayo aliyoyafunga kwa kushitukiza .
Alisema toka machimbo yalipofungwa maisha yao yamekuwa ni ya shida na wameanza kushindwa kutunza familia zetu kwani kwenye machimbo ndio walikuwa wakijipatia riziki ya kuendeshea maisha na kutunza familia zetu .
Silvester Mgema alieleza kuwa kupatikana kwa machimbo hayo ya Isumilomo kwa kipindi ambacho walikuwa wakichimba kumesaidia vijana wengi na waliacha kuzurula ovyo na pia waliacha kukaaa vijiweni na hata wizi umepungua katika Mji wa Mpanda .
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpanda alisema tamko hilo la kuwaondoa wachimbaji hao na kufunga machimbo hayo lipo kisheria kwa ajiri ya hali ya usalama wa afya kwa wachimbaji ambao walikuwa wamevamia eneo hilo ambalo lilikuwa linamilikiwa kihalali na watu kutoka kwa mmiliki wa eneo hilo TFS.
Alisema wachimbaji hao waliovamia eneo hilo walikuwa ni zaidi ya 400 na katika eneo hilo kulikuwa hakuna huduma zozote za muhimu kama vile vyoo na maji hivyo kulikuwa na hari ya kuhatarisha uwepo wa mlipuko wa magonjwa ya kipindupindu ,homa ya matumbo na kuhara damu .
Hivyo aliwataka wachimbaji hao wadogo wadogo kuwa wavumilivu na kutunza amani wakati wakisubiri maelekezo kutoka kwa wamiliki wa machimbo hayo .
Kwani yeye kama Mkuu wa Wilaya ametowa siku saba kwa wamiliki wa machimbo hayo kufanya marekebisho ya kufanya usafi kwani machimbo hayo yaliharibiwa na wachimbaji walivamia machimbo hayo ya Isumamilomo alisema DC Matinga .
MWISHO
No comments:
Post a Comment