Na Walter Mguluchuma.
Katavi .
Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozo Seif Idd leo yaani kesho anazindua mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2017 zitakazo zinduliwa Kitaifa Mkoani Katavi katika uwanja wa Mwenge Manispaa ya Mpanda .
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga maandaliza yote yashughuli zote ya uzinduzi wa mbio hizo za mwenge wa Uhuru yameisha kamilika .
Alisema kwa mwaka huu mbio hizo za Mwenge wa Uhuru zitazinduliwa na Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Idd na zitazinduliwa katika uwanja wa Mwenge uluoko katika Mtaa wa Ilembo Manispaa ya Mpanda .
Muhuga alieleza mara baada ya kuzinduliwa kwa mbio hizo mwenge wa Uhuru utakabidhiwa kwa viongozi wa Mkoa wa Katavi kwa ajiri ya kuukumbiza kwa siku tano katika Mkoa huo na kisha wataukabidhi Mkoa wa Rukwa .
Alisema kabla ya uzinduzi huo kutakuwa na kongamano la vijana litakalo washirikisha vijana wapatao 150 litakalofanyika katika katika ukumbi wa Halmashuri ya Manispaa ya Mpanda
litakalofunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera
,,, Bunge , Kazi , Vijana , Ajira na Watu mwenye ulemavu Jenista
Mhagama
Kongamano hilo litawashilikisha vijana mbali mbali ambao wametoka katika Halmashauri zote tano za Mkoa wa Katavi ambapo kila Halmashauri imetowa wawakilishi wa vijana hamsini hamsini .
RC Muhuga alisema katika Kongamano hilo vijana hao watafundishwa maada mbalimbali baadhi ya maada hizo ni ujasiliamali kupiga vita dawa za kuleya na ujumbe wa mbio za Mwenge wa Mwaka huu
MWISHO
No comments:
Post a Comment