Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Mkoani Katavi Sebastiani Kapufi amekabidhi msaada wa vitabu 390 Mi` saafu kwa viongozi wa Bakwata wa Mkoa wa Katavi akiwa na lengo la kutaka jamii ipatiwe eimu ya Dini ili iwe na hofu ya Mungu .
Msaada huo aliukabidhi hapo jana kwa Shehk Mkuu wa Bakwaka wa Mkoa wa Katavi Shehk Ally Hussein katika ofisi za Bakwata zilizopo katika Mtaa wa Majengo B pIa kwenye makabidiano hayo walihudhuria viongozi wa Bakwaka wa Wilaya zote za Mkoa wa Katavi .
Kabla ya kukabidhi vitabu hivyo Kapufi alieleza kuwa endapo jamii ya watu itapatiwa elimu ya dini itawafanya watu kuwa na hofu ya mungu na kuifanya nchi kuwa na amani na utulivu .
Alifafanua kuwa kuogoza jamii ya watu waio kuwa na hofu ya Mungu ni kazi kubwa na ndio maana viongozi wa dini wanayo nafasi kubwa ya kuelimisha jamii katika kuleta amani na utulivu .
Shekh Mkuu wa Mkoa wa Katavi Ally Hussein alimshukuru Mbunge huyo kwa msaada huo ambao alisema kuwa umefika kwa wakati kwani walikuwa na upungufu wa vitabu hivyo vya Dini .
Katibu wa Bakwata Wilaya ya Mpanda Omary Muna alieleza kuwa watahakikisha kutokana na msaada huo elimu inawafikia waumini na kuleta amani kwenye jamii .
Sudi Mbogo kiongozi wa kutoka msikiti wa Inyonga Wilayani Mlele alisema kuwa kiongozi huwezi kuongoza jamii bila kuwa na watu wenye hofu ya Mungu hivyo ni lazima watu wawe na hofu ya Mungu .
Vitabu hivyo vya Mi saafu vimegawiwa katika Wilaya za Mpanda, Tanyanyika na Mlele na vimepangwa kusambazwa katika Halmashauri zote tano za Mkoa wa Katavi .
MWISHO
No comments:
Post a Comment