Na Walter Mguluchuma .
Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Baraza la Madiwani la Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi limepitisha mapendekezo ya rasimu ya mpango wa Bajeti ya fedha kasi i cha zaidi ya shilingi bilioni 30.4 kwa ajiri ya mwaka wa fedha wa 2017\ 2018 zitakazo tokana na vyanzo vyake vya mapato ya ndani na ruzuku ya Serikali kuu na wafadhili mbalimbali.
Mapendekezo hayo ya rasimu ya bajeti ya Halmashauri hiyo yalipitishwa hapo jana na mkutano maalumu wa baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo ulioko katika Mtaa wa Ilembo .
Akisomo rasimu ya mapendekezo ya bajeti hiyo mbele ya Baraza la Madiwani Mkurugenzi wa Halmashauri Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu alieleza katika mwaka wa fedha wa 2017\ 2018 Halmashauri imekisia kukusanya kiasi cha cha jumla ya Tsh 30,493,088,000.
Nzyungu alifafanua kuwa fedha hizo ni zitatokana na vyanzo mbalimbali vya mapato ambapo mapato ya ndani wanatarajia kukusanya kiasi cha Tsh 2,378,800,000 na kiasi cha Tshs 28,114,288,000 ni ruzuku kutoka Serikali kuu na wafdhili mbalimbali .
Alsema makusanyo ya ndani katika Halmashauri hiyo yataongezeka kutoka Tshs 2,023,510, 000 hadi kiasi cha Tsh 2,378,000,000 sawa na ongezeko la asilimia 17.56 ya makisio ya mwaka wa fedha wa 2016\ 2017 ya Tshs 2,023,510,000.
Kuongezeka kwa makadirio ya mapato ya ndani ya Manispaa kumetokana hasa na ongezeko la makusanyo kutoka vyanzo vipya vya mapato ambavo hapo awali havikuwepo .
Nzyungu alivitaja vyanzo hivyo vipya mapato kuwa ni ushuru wa mabasi wa kituo kipya cha mabasi cha Ilembo kinachotarajia kuanza kazi mwezi Aprii mwaka huu pamoja na kukusanya mapato kwa njia ya mtandao.
Alisema Manispaa ya Mpanda imeandaa pia maombi maalumu kwa ajiri ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za idara ya Elimu msingi ,elimu sekondari , Aya na Ujenzi yenye gharama ya Tshs 7,525,169,860 maombi hayo yapo nje ya ukomo wa bajeti .
Meya wa Manispaa ya Mpanda Wiliy Mbogo alishauri kuwa utekelezaji wa bajeti hiyo ni vema ikalenga kwenye yale maeneo ambayo yanamatatizo makubwa ya kijamii.
Alisema yapo maeneo ambayo yanaupungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa hivyo ni vema kwenye maeneo hayo ndio yawe ya kwanza kupewa kipaumbele cha kwanza kuliko kupeleka bajeti ya kujenga madarasa kwenye maeneo ambayo hayana upungufu mkubwa .
Nae Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Liliani Matinga aliwataka wataalamu wa Manispaa hiyo wabuni vyanzo vipya vya mapato ya ndani ili fadha zitakazo patikana zisaidie kwenda kwenye shughuli za maendeleo ya jamii kuliko kukaa na kusubiria ruzuku ya serikali .
Aliwataka watumishi wa Halmashauri hiyo kutumia fedha vizuri za Serikali kulingana na jinsi zilivyokusudiwa kutumika na wasizitumie tofauti na matumizi yaliyokusudiwa .
MWISHO
No comments:
Post a Comment