Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Wafanya biashara wa kumbi za starehe na wamiliki wa bar na grosery wa Manispaa ya Mpanda wametekeleza maagizo ya jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi walioyatowa ya kupiga marufu kufanya disco la watoto kwenye kumbi zote za starehe na wenye bar na grosery kuzingatia sheria na kanuni kwa kuzingatia muda wa kufungua na kufunga na kutowahudumia vileo watoto wenye umri wa chini ya miaka 18.
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za matikio katika kipindi cha Sikuu ya Krismas ambayo yangeweza kuzorotesha ulinzi na usalama wa raia na mali zao Mkoani Katavi alitowa maagizo mbalimbali kwa wananchi na wafanya biashara wakati wa sherehe za krismas na maagizo hayo yametelezwa .
Miongoni mwa baadhi ya maagizo yaliotolewa na na kutekelezwa ni wamiliki wa kumbi za starehe kutopiga disco la watoto kama ambavyo ilivyokuwa kwenye sherehe za Krismas zilizopita.
Pia wamiliki wa Bar na grosery wamezingatia sheria na na kanuni za sehemu ya vileo kwa kuzingatia muda wa kufunga na kungua na walihakikisha usalama wateja wao na mali zao na wahakutowa huduma ya vileo kwa watoto waliochini ya umri wa miaka 18. Kama ambavyo walivyokuwa wameagizwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa huu.
Katika kipindi cha sikuu jeshi la polisi lilijipanga vyama na kuhakikisha linadumisha hali ya ulinzi na usalama kwa kufanya doria usiku na mchana katika maeneo yote hususani maeneo yenye kama kumbi za starehe , nyumba za ibada , kwenye makutano ya barabara na pia walifanya msako kwenye maeneo tete yenye viashiria vya uhalifu .
Mmoja wa wamiliki ya Bar ya Deluex iliyoko katika wa Majengo A Walter Malk alisema kuwa katika kipindi cha sikuu ya Krismas wameweza kufanya shughuli zao kama ambavyo jeshi la polisi lilivyokuwa limewaagiza wazingatie sheria za vinywaji na waliweza kufanya hivyo .
Nassor Arfi ambae ni Mwenyekiti wa wasafirishaji wa Mkoa wa Katavi alilipongeza jeshi la Polisi kwa uamuzi wake wa kupiga marufuku disco la watoto kwenye kumbi za starehe .
Alisema kitendo hicho kimesaidia kutokuwepo kwa watoto wanao dhurula ovyo mitaani kama ambavyo imekuwa kwenye sherehe zilizopita na pia imesaidia kupunguza ajari za barabarani kwa watu kugongwa na boda boda na baiskeli pia watoto kupotea.
No comments:
Post a Comment