Na Walter Mguluchuma Na Arine Temu
Katavi yetu Blog
Mji wa Mpanda Mkoani Katavi unakabiliwa na uhaba mkubwa wa mafuta ya petrol kwa kipindi cha siku tatu mfululizo na kupelekea lita moja ya mafuta kuuzwa kwa bei ya shilingi elfu saba badala ya bei elekezi ya Tsh 2070 na kupekekea bei ya vyombo vinavyo tumia mafuta hayo kupanda kwa kiasi kikubwa .
Wakiongea kwa nyakati tofauti na gazeti hili wendesha pikipiki Bodaboda wa vituo mbalimbali vya Manispaa ya ya Mpanda walisema wanalazimika kununua lita moja ya mafuta kwa bei ya Tsh 7,000 kwa lita moja badala ya bei elekezi ya Tsh 2070.
Mwenyekiti wa bodaboda wanaofanya shughuli zao katika kituo cha White Club Fericiani Masanja alieleza kuwa kwa siku ya tatu mfululizo vituo vya kuuza mafuta vya GBP na Allyen vikuwa haviuzi mafuta ya petrol kwa kile wanachodai kuwa mafuta hayo yamekwisha mpaka yaje mengine kutoka Dares salaam.
Alisema kutoka na kukosekana kwa mafuta kwenye vituo hivyo wanalazimika kununua mafuta hayo mitaani kwa bei ya kuluka ya Tsh 7,000 kwa lita moja badala ya Tsh 2070 kwa lita moja .
Boda boda wa kituo cha Soko kuu la Manispaa ya Mpanda Mawazo Bacho alieleza wamelazimika kupandisha nauli mara mbili kwa sehemu walizokuwa wakiwatoza abiria nauli ya Tsh 2,000 sasa wanawatoza Tsh 4,000.
Nae bodaboda wa stendi ya mabasi yaendayo Mikoani Liberatus Sigareti alisema mafuta hayo ambayo yamekuwa yakiuzwa mitaani ani na wafanya biashara wasio rasmi yanaweza kuhatarisha usalama wa watu kwani wakati wowote moto unaweza kutokea kwa jinsi mafuta hayo yalivyo hifadhiwa kwenye chupa na garoni .
Mwenyekiti wa Chama cha bodaboda Mkoa wa Katavi Stephano Asalile alisema toka mji wa Mpanda ukose huduma ya mafuta ya Petroli hari ya uchumi ya boda boda imehathilika kwani boda boda waliowengi wamesimama kufanya shughuli hiyo iliyokuwa ikiwaingizia kipato .
Alisema hata ukiangalia mitaani wananchi wamekuwa wakipata shida sana ya kupata usafiri kutoka na uchache wa bodaboda zinazofanya kazi tofauti na ilivyokuwa imezowelela .
Asalile aliiomba Serikali ya Mkoa kuingilia kati tatizo la kukosekana kwa mafuta ya Petroli katika Mji wa Mpanda kwani limekuwa ni tatizo la mara kwa mara alisema mwenyekiti huyo wa chama cha Bodaboda Mkoa wa Katavi
Mkazi wa Mtaa wa Kawajense Salome Mwanandenje alisema toka juzi analazimika kutembea kwa miguu kwenda kutafuta mahitaji baada ya kushindwa kulipia nauli aliyokuwa ameizowea ya Tsh 1,500 kutoka kawajense hadi soko kuu ambapo kwa sasa analazimika kulipa Tsh 3 ,000 kwa safari moja tuu ya kwenda
No comments:
Post a Comment