kaimu Kamanda Focas Malengo akionyesha
mbele ya Waandishi wa Habari meno mawili ya Tembo yenye thamani
ya milioni 30 aliyokamatwa nayo mtuhumiwa Asca Pius Mizengo
Mkazi wa Kijiji cha Nyakasi Tarafa ya Usevya Wilaya ya Mlele
Picha na Walter MguluchumaNa Walter Mguluchuma
Katavi yetu blog
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia Osca Pius Mizengo 30 Mkazi wa Kijiji cha Nyakasi Tarafa ya Usevya Wilaya ya Mlele kwa t uhuma za kukamatwa na meno mawili ya Tembo yenye uzito wa Kiligaramu 32 yenye thamani ya shilingi milioni 30 akiwa amehifadhi shambani kwake .
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Focas Malengo aliwaambia waandishi wa Habari jana kuwa mtuhumiwa alikamatwa juzi majira ya saa moja asubuhi huko katika kijiji cha Nyakasi Tarafa ya Usevya .
Aliwaambia Waandishi wa Habari kuwa mtuhumiwa alikamatwa kufuatia jeshi la Polisi kupata taarifa kutoka kwa Raia wema kuwa mtuhumiwa Osca anamiliki visivyo harali meno ya Tembo .
Baada ya taarifa hizo jeshi la polisi lilianza kufanya uchunguzi kuhusiaana na tuhuma hizo za kutoka kwa Raia wema wa Kijiji hicho cha nyakasi .
Kaimu Kamanda Malengo alisema ndipo ufuatiliaji ulipoanza kwa kufanyika upekuzi katika makazi ya mtuhumiwa Osca uliofanywa na Askari wa Jeshi la Polisi pamoja na viongozi wa Serikali wa Kijiji hicho .
Ndipo katika upekuzi huo polisi waliweza kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa amehifadhi meno ya Tembo mawili yenye thamani ya shilingi milioni 30 yenye uzito wa kilo 32 yakiwa yamefukiwa aridhini ndani ya shamba la mtuhumiwa.
Alisema meno hayo mawili ya Tembo yaliokamatwa moja lilikuwa na urefu wa sentimita 150 na jingine urefu wa sentimita 148 meno hayo wili ya Tembo ni sawa na Tembo hai mmoja .
Mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi na anatajiwa kufikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazo mkabili mara baada ya uchunguzi utakapo kuwa umekamilika .
Kaimu Kamanda ametowa Rai kwa wananchi kuacha kujihusisha na uharifu wa rasilimali za Taifa mfano vitendo vya ujangili nauwindaji haramu badala yake wafanye shughuli halali za kujipatia kipato.
No comments:
Post a Comment