Na Walter Mguluchuma
Katavi
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasilano Pro Makame Mbarawa amewaagiza wakandasi wote hapa Nchini waakikishe wanafanya kazi zao kwa wakati na kwakuzingatia viwango vinavyo takiwa .
Agizo hilo alilitowa hapo juzi wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Katavi kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi wakati wa ziara yake ya siku mbili Mkoani hapa .
Alisema lengo la Wizara yake ni kuwajengea Watanzania miundo mbinu ya kisasa ya kisasa hivyo wizara haiku tayari kuona mkandarasi anashindwa kufanya kazi kwa wakati na kwa kutozingatia viwango .
Waziri Mbarawa aliwaka wafanyakazi wa wakala za barabara hapa nchini Tanroods wafanye kazi kwa uadilifu mkubwa ili kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora na kasi inayotakiwa.
Alisema Serikali imeisha anza kuwalipa fedha wakandasi hivyo miradi ambayo ya ujenzi wa barabara iliyokuwa imesimama itaendela kama kawaida na itakamilika kama ilivyo kuwa imepangwa .
Kuhusu mawasiliano alisema Serikali itahakikisha maeneo yote ya pembezoni na mikani kuna kuwa na mawasiliano ya uhakika ukiwemo na Mkoa wa Katavi ambao baadhi ya maeneo mawasiliano ya simu hayapatikani .
Pro Mbarawa alieleza kuwa serikali imepanga kununua ndege mbili kwa ajiri ya shirika la ATC na wamepanga dende moja itakuwa inafanya safari zake katika Mji wa Mpanda Mkoani Katavi na Mikoa ya Kigoma na Dares salam kwani mikoa ya Katavi na Kigoma bado haina ushindani wa wa makampuni ya ndege .
Alisema uwanja wa ndege wa Mpanda uliojengwa kwa kiwango cha rami 1.8 unasifa zote za kutuwa kwa ndege ndogo hivyo wizara yake itaondoa changamoto inayoukabili uwanja ya ukosefu wa gari la zima moto hivyo gari hilo litapatikana hivi karibuni .
Alizungumzia reli ya Mpanda alisema usafiri wa treni kutoka Mpanda hadi Tabora hauta simama kwani Wizara imejipanga na kuhakikisha huduma hiyo inapatikana wakati wote na pia Serikali inampango wa kujenga reli kutoka Mpanda hadi Karema itakayokuwa inatumika kusafirishia mizogo hadi kwenye bandari inayojengwa katika Ziwa Tanganyika huko Karema na mizigo hiyo kuelekea Nchi ya Kongo.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Katavi Major Jenelali mstaafu Raphael Luhuga alimweleza Waziri huyo kuwa Mkoa huo unachangamoto kubwa ya barabara kuwa nyingi za udongo na changarawe kwani hadi sasa unabarabara ya rami kiasi cha kilometa 34 tuu hari ambayoimekuwa ikisababisha watu washindwe kusafirisha mazao yao .
Alisema kutokana na barabara hizo kuwa za udongo na changarawe zimekuwa zikiharibika sana hasa wakati wa masika na pia wanakabiriwa na changamoto ya uwanja wa ndege kukosa kituo cha kuongezea mafuta ya ndege katika uwanja wa ndege wa Mpanda na ndio inaweza ikawa sababu ya MKoa huo kukosa usafiri wa ndege.

No comments:
Post a Comment