Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Jumla ya watu ya watu 9,000 wamepima VVU Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi katika kipindi cha mwezi Oktoba hadi Desemba 2015 na wateja zaidi ya 300 waligundulika kua na maambukizi ya VVU ikiwa ni sawa na asilimia 3.5
Hayo yalisemwa hapo jana na mratibu wa kuthibiti ukimwi wa Wilaya ya Mpanda Dk Benald Kamande wakati akisoma taarifa ya utekelezaji huduma za ukimwi katika Wilaya ya Mpanda kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2015 mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima katika ofisi ya mganga mkuu wa Wilaya ya Mpanda.
Alisema idadi ya wateja waliopimwa VVU katika Wilaya hiyo na kupatiwa majibu yao ni 9,487 na idadi ya wateja waliogunduliwa kua na maambukizi ya VVU ni 334 sawa na asilimia 3.5
Dk vituoKamande alieleza katika kipindi hicho wateja wapya walioandikishwa katika vituo tiba na kupatiwa mafunzo ni 235. Na wateja wapya walionzishiwa dawa ARVs kwa kipindi hichi ni 187.
Mpaka sasa idadi ya wateja wanao dawa za ARVs hadi kufikia Desemba mwaka jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ni wateja 2186.
Alisema kumekuwapo na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa huduma za ukimwi Wilayani Mpanda baadhi
ya changamoto hizo ni utoro wa watumiaji wa dawa ARVs unasababishwa na
umbali wa vituo vya kutolea huduma na wateja wengine wamekuwa wakitumia
majina bandia.
Changamoto nyingine ni ukosefu wa usafiri wa gari la kutowa huduma za CTC na ukosefu wa umeme kwenye vituo na motisha mdogo kwa watowa huduma.
Nae mkuu wa kitengo cha CTC katika Halmashauri ya
Wilaya ya Mpanda Dr Benson Luhende katika kipindi hicho cha mizi mitatu
ya oktoba hadi desemba mwaka jana wateja 13 walifariki Dunia.
Alisema toka kituo kianze kutowa huduma wateja walioandikishwa ni 5521 kati yao wanaume ni 2348 na wanawake 3,173 na waliko kwenye ARVs ni wanaume 712 na wanawake 883.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima alisema kazi wanayofanya watumishi wa afya ni ngumu hivyo alimtaka mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya hiyo na Mganga mkuu kuangalia namna ya kuwapatia
motisha watumishi hao ili waendelee kuwa na moyo zaidi wa kufanya kazi .
Alisema motisha sio lazima
iwe ni kuwapatia fedha tuu mnaweza kufanya utaratibu wa kuwapeleka
watumisha hao kwenda kutembelea mbuga ya hifadhi ya Katavi au kuwapeleka
kwenda kuliona ziwa Tanganyika.

No comments:
Post a Comment