Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu blog
Muuguzi wa Zahanati ya Kapalamsenga Wilayani Mpanda Rehema Munga amenusurika kipigo na kupelekewa mwili wa marehemu nyumbani kwake baada ya wananchi wa Kijiji hicho kumtuhumu kuwa amesababisha kifo cha mgonjwa baada ya kukataa kumpatia huduma za matibabu wakati wa usiku.
Tukio hilo la muuguzi huo kutaka kupigwa na
kupelekewa mwili wa marehemu lilitokea hapo juzi majira ya saa kumi
usiku katika kijiji cha Kapalamsenga Tarafa ya Karema na kulazika nyumba ya mganga huyo kuwa chini ya ulinzi wa askari wa jeshi la Wananchi wa Tanzani wa Kikosi cha Ikola.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Hamad Mapengo aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa wananchi
hao walipandwa na hasira baada ya kumtuhumu mganga huyo kuwa
amesababisha kifo cha Bibiana Karangi 49 kwa kuchelewa kumpatia huduma
za matibabu kwa wakati.
Alisema siku hiyo ya tukio majira ya saa saba usiku
marehemu huyo alifikishwa katika zahanati hiyo na walipohitaji huduma
ya matibabu kwa kumwamsha mganga huyo aliyekuwa nyumbani kwake kwenye
eneo la zahanati hiyo alikataa kuamka na aliwataka wampeleke mgonjwa huyo katika kituo cha afya cha Karema .
Mwenyekiti huyo alieleza mgonjwa
huyo alipelekwa hadi kwenye kituo cha afya Karema na kugundulika kuwa
anatatizo la upungufu wa damu hivyo anatakiwa apelekwe katika Hospitali
ya Wilaya ya Mpanda na wakati akiwa hapo alifariki baada ya muda si
mrefu .
Baaada ya Bibiana kufariki Dunia baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kapalamsenga walipata taarifa ya kifo hicho na ndipo walipoamua kujikusanya kwa lengo la kwenda kituo cha afya cha Karema ili wakachukue mwili wa marehemu na kuupeleka chumbani kwa mganga wa zahanati hiyo kwa kile walichodai kuwa ndiye aliyesababisha kifo hicho kwa kutompatia huduma na mapema .
Viongozi wa Kata hiyo walipata taarifa hizo hari
ambayo iliwalazimu waombe msaada kwa askari wa Jeshi la wananchi wa
kituo cha ikola ambao walifika kwenye eneo hilo na kuizingira nyumba ya mganga wa zahanati hari ambayo iliwalazimu wananchi hao kuanza kutawanyika kwenye eneo hilo .
Hamad Mapengo alieleza kuwa ilimlazimu yeye na kaimu mganga mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dk Naibu Mkongwa wachukue uamuzi wa kwenda kumchukua mganga huyo na kumpeleka Mpanda Mjini kwa kuhofia hari ya usalama wake.
Afisa Tarafa wa Karema Zawadi Mirambo jana alilazimika kwenda kijijini hapo na kufanya kikao na wananchi hata hivyo kwenye kikao hicho maoni ya wananchi hao yalitofautiana na
wauguzi wa zahanati hiyo ambapo wauguzi walidai kuwa marehemu huyo
alikuwa meisha ugua muda mrefu na alikuwa ameisha ambiwa akatibiwe
kwenye kituo cha afya cha Karema toka muda mrefu .
Wananchi wao walidai kuwa imekuwa ni kitendo cha mara kwa mara mganga huyo kukataa kutowa huduma kwa wagonjwa nyakati za usiku kutokana na hari yake ya ujauzito.
Kabla ya kikao hicho cha afisa Tarafa na wananchi Mtendaji wa Kata hiyo aliokota barua ambayo
ilandikwa na watu wasiojulikana ikiwa inaeleleza kuwa mganga huyo
hawataki kumwona tena akitowa huduma kwenye zahati hiyo na wala
asionekane tena kijijini hapo .
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda
ameunda tume ya kufatila tatizo hilo ilikuweza kupata ukweli kuhusiana
na tuhuma za wananchi .

No comments:
Post a Comment