Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu Blog
Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Zuhura Salumu 34 Mkazi wa Mtaa wa Majengo Wilaya ya Mpanda amejeruhiwa kwa kuchomwa na kisu katika titi lake la kulia wakati akiwa wakiwa wamelala na mpenzi wake kwenye nyumba ya kulala wageni inaitwa Maridadi iliyoko katika Mtaa wa Majengo B mjini Mpanda.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema mbele ya waandishi wa Habari kuwa tukio lilitokea hapo juzi katika nyumba ya kulala wageni inayoitwa Maridadi katika Mtaa wa Majengo.
Alisema siku hiyo ya tukio Zuhura alikuwa amelala kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni huku akiwa amelala na mpenzi wake anaitwa Iddy Salehe.
Kamanda Kidavashari wakati wakiwa wamelala mtuhumiwa Iddy Salehe aliamka na kumvizia Zuhura wakati akiwa usingizini na kumchoma kisu kwenye titi lale la kulia na kumjeruhi vibaya.
Alieleza kitendo
hicho kilimfanya Zuhura apige mayowe ya kuomba msaada na aliweza
kusaidiwa na walinzi wa nyumba ya kulala wageni hiyo na ndipo
walipofanikiwa kumkamata mtuhumiwa na waliweza kutowa taarifa polisi
ambao walifika kwenye eneo hilo baada ya muda mfupi.
Kidavashari alisema chanzo cha tukio hilo bado akijajulikana mpaka sasa kilichopelekea mtuhumiwa kufanya kitendo hicho kisicho cha kawaida.
Mtuhumiwa Iddy Salehe bado anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi na anatarajiwa kufikishwa Mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.
No comments:
Post a Comment