Friday, January 22, 2016

TAKUKURU YAMFIKISHA KIZIMBANI AFISA MTENDAJI WA MTAA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
  Katavi
 Taasisi ya kuzuia na kupambana na  Rushwa (Takukuru) Mkoani Katavi imemfikisha Mahakamani  Afisa Mtendaji wa Mkoa wa Kawajense Manispaa ya Mpanda  Catherine Kipeta kwa  tuhuma za kumkamata  za kushawishi  na kuomba Rushwa ya  Tsh 30,000.
Kaimu  Mkuu wa Takukuru Mkoa  wa Katavi  Cristopher Nakua  aliwaambia waandishi wa Habari jana  kuwa  Afisa Mtendaji huyo alikamatwa  hapo january 18 mwaka huu katika eneo la Mtaa wa Kawajense Mjini hapa.
 Alisema  mtuhumiwa alikamatwa kufuatia  Ofisi ya Takukuru kupokea taarifa  kutoka kwa msiri wao  aliyemtuhumu  Afisa Mtendaji  wa Mtaa wa Kawanjense  Catherine Kipeta  kuwa amemwomba na kumshawishi  ampe Rushwa  ya kiasi cha Tsh 30,000 ili asiweze  kumpeleka  kwenye Baraza la Kata  kwa kosa  la kufungua sehemu yake ya biashara katika muda wa kufanya usafi .
Baada ya   kupokea taarifa hizo  ofisi ya Takukuru  ilifanya  uchunguzi  na baada ya  kuthibitika kuwepo kwa tuhuma hizo  ndipo  mtego  wa Rushwa  ulipoandaliwa  na walipoweza  kumkamata  Catherine Kipeta ambae ni  Afisa Mtendaji  wa Mtaa wa Kawajense baada ya kuwa amepokea  Rushwa aliyokuwa  ameiomba  kutoka kwa msiri huyo.
Nakua aliwaeleza waandishi wa Habari  kuwa mshitakiwa   alifikishwa juzi  katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda  na kufunguliwa  kesi  No.CC 12- 2016.
Na  mtuhumiwa  alisomewa mashitaka  ambayo ni  kuomba Rushwa  ya fedha tasilimu Tsh 30,000 shitaka la pili alilosomewa ni  kupokea  Rushwa ya  shilingi elfu salasini  kinyume  na matakwa  ya mwajiri wake  kifungu  cha 15 (1) (a) cha sheria  ya kuzuia  na kupambana na RushwaNa 11 ya mwaka  2007.
Takukuru Mkoa wa Katavi  wametowa wito  kwa wananchi  wote  wajiepushe na vitendo vya Rushwa  ambavyo hupelekea kutopatikana kwa haki , kutowajibika kwa watumishi wa umma na kwenda kinyume na maadili  ya kanuni  na viapo vya utumishi.

No comments:

Post a Comment