Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Mahakama ya
Wilaya ya Mpanda Imewahukumu watu wawili
kifungo cha miaka 42 jela baada
ya kupatikana na hatia ya kukamatwa na meno ya Tembo manne yenye thamani ya shilingi milioni sitini
Hukumu hiyo
ilitolewa hapo jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Odira
Amwol baada ya mahakama kulidhika na ushahidi uliotolewa Mahakama na
upande wa mashitaka.
Watuhumiwa hao waliohukumiwa kifungo hicho cha
kwanda jela ni Justine Bruno(50) Mkazi wa Kijiji cha Usevya na
Filiberti Leo(35) Mkazi wa Kijiji cha Ikuba wote
wawili wakazi wa Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi.
Awali katika kesi
hiyo mwendesha mashitaka mwanasheria wa Serikali Jamila Mziray
aliiambia Mahakama kuwa watuhumiwa hao wote
wawili walikamatwa na meno ya tembo hapo Novemba 17 mwaka huu majira ya
usiku katika kijiji cha Ikuba Wilayani Mlele.
Siku hiyo ya tukio watuhumiwa hao walikamatwa na
Askari wa jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi
kwa kushirikiana na Askari wa TANAPA wa Mbuga ya Katavi huku wakiwa wamepakia
kwenye pikipiki meno ya Tembo manne yenye
uzito wa kilogramu 47.6 yenye thamani ya shilingi milioni sitini.
Upande wa
mashitaka katika kesi hiyo ulikuwa na mashahidi watano na
washitakiwa walikuwa hawana shahidi
yoyote hivyo walijitetea wenyewe .
Hakimu Amwol
kabla ya kusoma hukumu hiyo aliiambia Mahakama kuwa kutokana na mwenendo
mzima wa kesi hiyo mahakama pasipo shaka yoyote imewatia washitakiwa hatiani hivyo kabla ya kutolewa kwa hukumu anawapa nafasi washitakiwa kama wanasababu yoyote ya msingi ya
kuishawishi mahakama iwapunguzie adhabu anatowa nafasi kwa washitakiwa kujitetea.
Washitakiwa
katika utetezi wao waliiomba Mahakama iwapunguzie adhabu kwa kuwa
wanawazazi na watoto ambao wanaowategemea .
Mwanasheria wa
Serikali alipinga vikali maombi hayo na kuiomba mahakama itowe adhabu kali kwa
washitakiwa kwani tatizo la ujangili
katika Mkoa wa Katavi limekuwa likiongezeka siku hadi siku hivyo wapewe adhabu
ambayo itakuwafundisho na kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.
Akisomo hukumu hiyo Hakimu Amwol aliiambia Mahakama kuwa washitakiwa wamepatikana na kosa la kuvunja sheria ya
uwifadhi wa wanyama kifungu
86(1) 2b na c na kifungu cha
sheria cha makosa ya kupanga
na kuhujumu uchumi No 57 (1)(60) sura ya 200 marejeo ya 2002.
Hivyo kutokana na
kupatikana na kosa hilo Mahakama imewahukumu
Justine Bruno na Filiberti Leo
kutumikia kifungo cha miaka 21 jela kwa kila mmoja .
No comments:
Post a Comment