Tuesday, December 8, 2015

HOT NEWS: NDUGU WA MAREHEMU WAKATAA KUMZIKA NDUGU YAO ALIYEPIGWA RISASI NA ASKARI WA TANAPA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter Mguluchuma
Katavi yetu Blog
Mwili wa Mfugaji wa mifugo  Moshi  Salehe (17) Mkazi wa Kijiji cha  Kamsisi Wilaya ya  Mlele  Mkoani hapa umeshindwa kuzikwa na ndugu zake na bado unahifadhiw katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa muda wa siku tatu sasa  baada ya baba mzazi wa marehemu  na ndugu zake  kukataa kuuzika  kwa kila wanachodai  mpaka hapo watakapo kuwa wamechukuliwa hatua Askari wa wanyama pori wa TANAPA wanaosadikiwa kumuuwa kwa kupiga risasi
Kwa mujibu wa baba mazazi wa marehemu   Samweli  Daki  aliwaambia jana waandishi wa habari kwenye    jengo la  kuhifadhia  maiti la hospitali ya Wilaya ya Mpanda kuwa marehemu mtoto wake alifariki Desemba 6  majira ya saa kumi jioni  katika  eneo la Kanono wilayani  Mlele
 Alisema kuwa siku hiyo ya tukio yeye akiwa na marehemu na watoto wake wengine watano walikuwa wakiswaga Ng’ombe zao kutoka Kata ya  Mpanda ndogo Wilaya ya Mpanda wakiwa wanaelekea  Kijiji cha  Kamsisi  Wilayani  Mlele walikokuwa wanahamishia  makao yao
 Alieleza ndipo walipofika kwenye eneo hilo ambapo marehemu alikuwa akiswaga   ng’ombe hizo  kwenye  kichaka  alipokutana  na  askari hao wa TANAPA  wa hifadhi ya Katavi waliokuwa dolia kwenye gari lao  na  walianza kuwafyatulia risasi na ndipo    risasi moja ilipo  mpiga  marehemu kwenye paja lake huku wale alikuwa nao  msafara mmoja waliamua wao kutokomea
 Samweli  alieleza baada ya kuwa wamempiga risasi hiyo askari hao waliondoka na kumwasha  porini bila kumpatia msaada wowote ule na waliondoka na gari lao kuelekea njia ya kwenda Mpanda Mjini
Baada ya muda     walikwenda kwenye eneo hilo na kumchukua marehemu na  kumsogeza barabarani kwa ajiri ya kupata msaada wa kummpeleka hospitali  hata hivyo  alifariki baada ya muda  kutokana na kuwa amevuja damu  nyingi
Kwa  upande wake Mwenyekiti wa wafugaji wa Wilaya ya Mlele  Zenge  Luhanga  alieleza kuwa  anaungana na ndugu wa marehemu  kuwaunga mkono kwa uamuzi wao wa kutokubali kuzika mwili wa marehemu mpaka wahusika wa tukio watakapo kuwa wamechukuliwa hatua
 Alisema  wako tayari kushirikiana na ndugu wa marehemu hata kama itakuwa ni mwezi mzima   huhakikisha mwili wa marehemu auzikwi mpaka watuhumiwa watakapo kuwa wamekamatwa
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi   Rashid  Mohamed  alikiri kutokea kwa kifo cha marehemu huyo ambae ni mfugaji wa mifugo
Alisema  marehemu huyo aliuwawa kwa kupigwa risasi na Askari wa wanyama pori waliokuwa wakifanya doria
Kaimu  Kamanda Rashid Mohamed  alisema jeshi la polisi Mkoa wa Katavi limeisha chukua hatua kwa  kuwakamata na linawahoji Askari wa Wanyama Pori wa TANAPA walitajwa kuhusika katika tukio hilo

No comments:

Post a Comment