Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Waumini wa Kanisa
la Kiijili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Ziwa Tanganyika inayounda Mikoa
ya Katavi na Rukwa imepanga kufanya
ibada ya misa Oktoba 24 badala ya
Oktoba 25 ilikuwapa nafasi waumini wa Kanisa hilo kushiriki uchaguzi
mkuu utakao fanyika Jumapili ya oktoba 25
Hayo yalisemwa
hapo jana na Askofu wa KKT Dayosisi ya
Ziwa Tanganyika wakati alipokuwa akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu
wakati akiwa Sumbawanga Mkoa wa Rukwa
Alisema Kanisa limeamua kuhamishia
ibada hiyo siku ya juma mosi
badala ya jumapili ili kutowa nafasi kwa waumuni wa Kanisa hilo kushiriki kakamilifu uchaguzi mkuu wa Oktoba 25
Kanisa
linatambua umuhimu wa uchaguzi Mkuu ndio
maana limehamisha shughuli zake zote ambazo zilikuwa zifanyike jumapili ya Oktoba 25 na badala yake
zitafanyika jumamosi ya oktoba 24
Nae Katibu wa
Dayosisi hiyo Abrahamu Kombe amesema
kuwa Kanisa limefanya jambo zuri sana kuhamishia ibada siku hiyo ya jumamosi badala ya
jumapili
Alisema hakuna tena muumini wa Kanisa hilo
Katika Dayosisi ya Ziwa Tanganyika ambae
atashindwa kupiga kura kwa kisingizio
cha kuwa alikuwa kwenye ibada
Mpaka saa kuna baadhi ya Madhehebu ya Dini
mbalimbali hapa nchini
wameishatangaza kuhamishia ibada zao siku ya jumamosi ya tarehe 24 badala ya tarehe 25 oktoba kwa
ajiri ya kupisha uchaguzi mkuu utakaofanyika siku hiyo wa kuwachagua Wabunge na
Madiwani na Rais
No comments:
Post a Comment