Friday, August 21, 2015

HOT NEWS: CHADEMA YAMUENGUA MGOMBEA UBUNGE ALIYETEULIWA NA WILAYA BADALA YA KAMATI KUU YA CHAMA HICHO NA TAYARI ALIKUWA AMEISHA CHUKUA FOMU TUME YA UCHAGUZI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi yetu Blog
Chama  cha  Demokrasia na Maendeleo  (CHADEMA) Mkoa wa Katavi kimemuengua  mgombea wake wa kugombea Ubunge wa Jimbo la Kavuu Mkoa wa Katavi Amos  Mayala  ambae  alikuwa  amechukua fomu kwa msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Kavuu kwa kile kinachodaiwa kuwa  uteuzi wake uliofanywa na ngazi ya Wilaya ni kinyume na taratibu za Chama hicho
Katibu wa CHADEMA  wa Mkoa wa Katavi   Almasi  Ntije  alisema  kuwa   uamuzi wa kumwengua   Amos Mayala  ulifanywa  jana  na viongozi wa  chama  hicho wa Mkoa wa  Katavi  baada ya kubaini kuwa uteuzi wake ulifanywa kimakosa  na viongozi wa   Chama  hicho wa Wilaya ya Mlele
 Alisema  chama  hicho  kimemteuwa  Laulenti  Mangweshi kuwa ndio  mgombea wa  Ubunge kupitia  umoja wa UKAWA kama   ambavyo  kamati kuu ya  CHADEMA  ilivyokuwa imemteuwa  Mangweshi  kuwa  ndio  mgombea wa ubunge wa Jimbo hilo (CHADEMA)
Alifafanua kuwa viongozi wa   CHADEMA wa Wilaya  ya  Mlele  hawakuwa na mamlaka ya kumteuwa Mayala kuwa ndio mgombea wa Jimbo hilo  kwani  taratibu za  chama  hicho uteuzi wa wagombea  ubunge  hufanywa na  kamati kuu ya  Chama hicho
Ntije  alisema   baada ya kuwa wamegundua uteuzi huo ulikuwa na  kasoro walimwandikia  barua  msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Kavuu wa kuliondoa  jina   na  Amos   Mayala  na  badala yake mgombea  halali wa  chama hicho ni  Mangweshi
 Alisema  ingawa  hapo awali  baada ya  Amos  Mayala  kuandikiwa  barua  na  viongozi wa chama  hicho wa Wilaya ya Mlele ya kumtambulisha kwa msimamizi wa uchaguzi  kuwa  ndio mgombea wao  msimamizi wa uchaguzi  alimkabidhi  fomu za  kugombea  ubunge wa Jimbo hilo na kisha  alikwenda  mahakamani  na kuapa kiapo  hivyo  Chama  hicho kilifanikiwa kumuwahi kabla haja rudisha  fomu hizo
Katibu  huyo wa  Chadema wa Mkoa wa Katavi  alieleza  kuwa   jana walifanikiwa kukamilisha taratibu za  kuchukua fomu za mgombea wao wa Ubunge wa Jimbo la Kavuu Laulenti Mangweshi na mara baada ya kukamilisha taratibu hizo  fomu hizo zilikabidhiwa na kupokelewa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Katavi Godwin Bene
Katika kura za maoni za chama hicho  Mangweshi alikuwa ni mshindi wa kwanza na  Mayala  alikuwa ni mshindi wa pili   na uteuzi uliofanywa hivi karibu na  kamati kuu ya  Chadema ulimteuwa  Laulenti  Mangweshi kuwa ndio  mgombea wa jimbo la Kavuu

No comments:

Post a Comment