Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Juma
Chum amewataka Watanzania kutowachagua viongozi wanao taka
wachaguliwe kuongoza kwa kutumia Rushwa na badala yake wawachague viongozi bora
na waleta maendeleo
Chum alitowa
kauli hiyo hapo
juzi wakati alipokuwa akiwahutubia
mamia ya wanachi wa Tarafa ya I
Inyonga Wilaya ya Mlele
Mkoa wa Katavi wakati wa siku ya
mwisho ya mbio za mwenge uliokimbizwa
katika Mkoa wa Katavi kwa muda wa
siku nne
Alisema wapo
baadhi ya viongozi ambao wanataka
kuchaguliwa kuongoza kwa njia ya kuwapatia wananchi Rushwa ili
wawachague
Alifafanua kuwa wapo baadhi
ya viongozi ambao wamekuwa
wakitaka wachaguliwe kwa njia ya Rushwa na matokeo yake baada ya kuchaguliwa wamekuwa wakishindwa
kuwaletea wananchi maendeleo kwenye maeneo yao
Hivyo ni budi
watanzania wakajitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura za kuwachagua
viongozi kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba
25 na wawachague viongozi wale ambao watawaletea maendeleo
Pia
aliwataka wa wanafunzi wa shule
za Sekondari hapa nchini wasome kwa bidii na kuachana na tabia
ya kupata mimba za utotoni kwani hazina
manufaa kwenye maisha yao
Alisema
wa wapo baadhi ya wazazi wamekuwa
na tabia ya kuwazosha watoto wao na kuwakatisha masomo hivyo
wanafunzi hao wajenge tabia ya
kuwakatalia wazazi wao kuwakatisha masomo ili waolewe
Mbio za mwenge
zimelaliza mbio zake za siku nne
katika Mkoa wa Katavi hapo jana ambapo
jumla ya miradi yenye thamani ya ziidi ya shilingi Bilioni nne ilizinduliwa na kuwekwa jiwe la msingi
katika Mkoa wa Katavi na jana Mwenge wa Uhuru ulikambiziwa kwa
viongozi wa Mkoa wa Tabora
No comments:
Post a Comment