Monday, July 13, 2015

HALMASHAURI YA MJI WA MPANDA YAPOKEA ZAIDI TSH MILIONI 437 ZA MATENGENEZO YA BARABARA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Halmashauri ya  Mji wa   Mpanda  Mkoa  wa  Katavi  ambayo  imepandishwa  hivi  karibuni  kuwa  Halmashauri ya Manispaa  hadi  kufukia june 30  mwaka huu  ilikuwa  imepokea  kiasi  cha  zaidi ya  shilingi  milioni  437   kwa  ajiri ya matengenezo  ya barabara  zake  kwa mwaka wa fedha wa 2014 na 2015
 Hayo  yalisemwa hapo  juzi na  Mwenyekiti  wa  Halmashauri  ya  Mji wa  Mpanda   Enock  Gwambasa  wakati wa kikao cha  mwisho  cha  baraza  la  Madiwani  wa  Halmashauri  hiyo  kilichofanyika  katika  ukumbi waHalmashauri ya  Manispaa ya  Mpanda 
 Alisema  katika  mwaka  wa  fedha wa 2014  na 2015 Halmashauri  hiyo  ilitenga  kiasi  cha  shilingi  Bilioni    moja milioni  mia  moja  ishirini  na moja  na miatano  elfu  kwa ajiri  ya matengenezo  ya  aina  mbalimbali  ya  barabara  kutoka  mfuko wa  barabara (ROAD FUND )
 Alifafanua  hadi kufikia  june  30  mwaka huu   Halmashauri yake  ilikuwa imepokea  kutoka  Serikalini  kiasi  cha   jumla ya  Tsh 437,565,635.16  ambazo ni sawa na  asilimia  39 ya  bajeti yake yote  ya matengenezo ya barabara  kwa  mwaka fedha wa 2014 na 2015
 Alisema    hadi  kufukia  june   30    mwaka huu  Halmashauri ya  ilikuwa  imeingia  mikataba  saba  ya  matengenezo ya  Barabara  yenye  gharama  ya Tsh 632,924,000 kwa ajiri ya matengenezo ya  barabara za mji wa Mpanda
Gwambasa alielez a  katika utekelezaji wa  kazi za barabara  kumekuwepo na changamoto  mbalimbali   ambazo  zimekuwa zikijitokeza 
 Alizitaja  baadhi ya  changamoto hizo  kuwa ni  makandarasi  wengi  walioko  Mkoa wa Katavi  hawana  mitambo  yao kwa  matengenezo  ya  barabara  na badala yake  hutegemea  mitambo  ya kukodi  kitu  ambacho hufanya  kuchelewa kuanza  utekelezaji w kutengeneza barabara
 Changamoto  nyingine  aliitaja kuwa ni  fedha  zinazotengwa  kwa mwaka  kwa ajiri ya matengenezo ya barabara  ni kidogo hivyo hazitoshelezi mahitaji  halisi
Pia   makandarasi wengi  hawana  mitaji ya kutosha  hivyo  huwafanya  washindwe kuanza kazi kwa wakati unaokuwa umepangwa

No comments:

Post a Comment